Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MY DREAM BARBERSHOP YATWAA TENA TUZO YA BARBERSHOP BORA MKOA WA SHINYANGA

My Dream Barbershop imeendelea kuandika historia katika sekta ya huduma za urembo na unyoaji baada ya kutwaa tena tuzo ya Barbershop Bora Mkoa wa Shinyanga, na kufanya hivyo kwa mara ya pili mfululizo.

Mafanikio hayo yanaendelea kuimarisha nafasi ya My Dream Barbershop kama moja ya chapa zinazotambulika katika sekta ya unyoaji, huku yakidhihirisha dhamira ya kampuni hiyo katika kutoa huduma bora, kukuza vipaji vya vijana na kutengeneza fursa za ajira.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Juma Diwani, Mkurugenzi wa Mipango na Masoko wa My Dream Barbershop, amesema kuwa ingawa tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa kampuni, mafanikio yenye thamani zaidi ni kuona vijana wakipata ajira, kukuza vipaji vyao na kujitegemea kiuchumi.

“Tuzo ni heshima kubwa kwetu, lakini kuona vijana wakipata ajira, kukuza vipaji vyao na kusimama kwa miguu yao wenyewe ndiyo fahari yetu kubwa zaidi,” alisema Diwani.

Ameongeza kuwa kupitia matawi mawili ya My Dream Barbershop, kampuni hiyo imefanikiwa kutengeneza ajira za moja kwa moja kwa vijana zaidi ya 100, sambamba na kuchochea ajira nyingine nyingi zisizo za moja kwa moja.

“Kwetu, haya ndiyo mafanikio makubwa zaidi kuona ndoto zikikua, vipaji vikipewa nafasi na maisha yakibadilika kupitia fursa tunazotengeneza,” alisisitiza.

Kauli hiyo inaonesha falsafa ya My Dream Barbershop katika kuunganisha ukuaji wa biashara na maendeleo ya jamii, hasa kwa kuwapa vijana nafasi ya kutumia vipaji vyao, kupata kipato na kujenga maisha yenye matumaini.

Kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo ni hatua muhimu kwa kampuni hiyo, huku kukiwa na matarajio ya kuendelea kuboresha huduma, kuimarisha chapa yake na kupanua fursa zaidi kwa vijana.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com