Na Mbuke Shilagi Kagera
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, Dokta Peter Mkenda, amewataka wananchi kuchukua tahadhari za kiafya dhidi ya ugonjwa wa Ebola, kufuatia taarifa za kuripotiwa kwa maambukizi ya ugonjwa huo nchini Kenya.
Mkenda ametoa wito huo akiwa ofisini kwake akizungumza na Malunde Blog, amesisitiza umuhimu wa wananchi kutambua dalili za ugonjwa huo na kutoa taarifa mapema kwa mamlaka za afya ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Ameeleza kuwa dalili zinazoweza kuashiria Ebola ni pamoja na homa kali ya ghafla, uchovu mkubwa, maumivu ya misuli na kichwa, kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi na kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili.
Aidha, amewataka wananchi kuepuka kugusa mizoga ya wanyama, damu na majimaji ya mwili wa mtu anayeshukiwa kuwa na maambukizi, pamoja na kutowahudumia wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na Ebola bila vifaa na taratibu sahihi za kujikinga.
Mkenda amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutoa taarifa haraka wanapobaini mtu mwenye dalili zinazotia shaka, badala ya kusubiri hali yake kuwa mbaya zaidi.
Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya na kupunguza mikusanyiko isiyo ya lazima kama sehemu ya kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
Amewahimiza wananchi kutosambaza taarifa zisizothibitishwa na badala yake kushirikiana na mamlaka za afya katika kulinda usalama wa jamii.

Social Plugin