Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAIPONGEZA TRA KWA UFANISI WA MAKUSANYO NA MATUMIZI YA MIFUMO YA KIDIJITALI

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda (aliyesimama) akiwasilisha jambo wakati wa semina ya mafunzo ya mifumo ya IDRAS, TANCIS na mfumo wa uondoshaji mizigo Bandarini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Mashimba Ndaki (aliyekaa mbele) bungeni jijini Dodoma.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda (aliyesimama) akiwasilisha jambo wakati wa semina ya mafunzo ya mifumo ya IDRAS, TANCIS na mfumo wa uondoshaji mizigo Bandarini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Mashimba Ndaki (aliyekaa mbele) bungeni jijini Dodoma.

Pichani ni baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakifuatilia wasilisho wakati wa semina ya mafunzo ya mifumo ya IDRAS, TANCIS na mfumo wa uondoshaji mizigo Bandarini kwa Kamati hiyo yaliyofanyika leo 15.10.2026 bungeni jijini Dodoma.

***

Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kwa ufanisi katika ukusanyaji wa mapato bila kuvutana na wananchi na matumizi ya mifumo ya kidijitali. 

Akizungumza wakati wa semina ya mafunzo kuhusu mfumo wa usimamizi wa kodi za ndani (IDRAS), mfumo wa Forodha TANCIS na mfumo wa uondoshaji mizigo Bandarini iliyotolewa kwa Kamati hiyo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiongozwa na Kamishna Mkuu Bw. Yusuph Juma Mwenda, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mashimba Ndaki amesema kazi nzuri inayofanywa na TRA inaipeleka Tanzania kwenye kujitegemea kiuchumi kwa kiasi kikubwa. 

Amesema kila wakati TRA inapopewa malengo na Serikali imekuwa ikiyavuka na kutolea mfano makusanyo ya kodi ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo TRA imekusanya kiasi cha Sh. Trilioni 10.65 sawa na asilimia 107.49 ya lengo la kukusanya Sh. Trilioni 9.91kiwango ambacho ni kikubwa kuwahi kukusanywa kwa kipindi kama hicho. 

Amesema semina waliyopewa na TRA kuhusu matumizi ya mifumo ya kidijitali ya IDRAS, TANCIS na uondoshaji mizigo Bandarini yamewaongezea uelewa huu ya kazi za TRA hali itakayowawezesha kufuatilia kwa karibu na kusimamia masuala yanayohusiana na ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema TRA inaendelea kujiimarisha kimifumo ili kurahisisha ulioaji kodi na kuwa wametoa semina hiyo ya mafunzo kwa Wabunge ili kuwawezesha kuwa mabalozi wazuri wa ukusanyaji wa mapato.

Mwenda amesema mifumo ya kodi kwa kiasi kikubwa imeboresha utawala wa kodi na kupunguza kuonana kwa watumishi wa TRA na walipakodi pamoja na kuongeza uwazi katika ukusanyaji wa kodi.

Amesema kuwa idadi ya Walipakodi nchini imefikia 9,000,000 ikihusisha Waajiriwa, Wafanyabiashara na wawekezaji ambapo kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 TRA imesajili Walipakodi wapya zaidi ya 447,000 hali iliuochagizwa na msamaha wa kodi kwa biashara mpya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com