Na Mwandishi Wetu
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CRJE (E.A) LTD na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makampuni ya Kichina Nchini Tanzania (CEAT), Bw. Jiang Yuntao, wakati akizungumza katika Jukwaa la Maendeleo ya Kimataifa la Makampuni – Tanzania (Phoenix Global Development Forum for Enterprises–Tanzania), lililofanyika Oktoba 3, 2026 katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
Bw. Jiang alisema mafanikio hayo ni sehemu ya mchango wa CRJE katika kuimarisha misingi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia miundombinu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba, barabara, viwanja vya ndege, umeme, maji, umwagiliaji, bandari na uwekezaji.
Jukwaa hilo liliandaliwa kwa pamoja na Phoenix TV na CEAT kwa kaulimbiu ya "Kugundua Afrika Mpya, Kuchunguza Fursa Mpya," na kuhudhuriwa na wageni takriban 100 kutoka serikalini, sekta binafsi na vyuo vikuu, akiwemo Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji; Bw. Shigeki Komatsubara, Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania; na Mhe. Chen Mingjian, Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania.
Alieleza kuwa historia ya CRJE nchini Tanzania inaanzia kwenye Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA) mwaka 1969, ambapo kampuni mama yake CRCEG ilituma wafanyakazi 1,114 kujenga mita za mraba 506,400 ikiwemo vituo 93, na mwaka 2000 ikasajiliwa rasmi Dar es Salaam – mwaka ule ule wa Dira ya 2025 – na mwaka 2013 kuwa CRJE (E.A) LTD.
Alisema kampuni sasa imejipanga kuunga mkono DIRA 2050 iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Julai 2025 inayolenga Tanzania yenye ustawi, haki, ushirikishwaji na kujitegemea ifikapo 2050.
Miongoni mwa miradi mingine aliyoitaja ni hoteli za nyota tano kama Kilimanjaro Hotel Dar, Gran Melia Arusha na Park Hyatt Zanzibar, Daraja la Nyerere kati ya Kurasini na Kigamboni, Bandari ya Mtwara, mradi wa umwagiliaji Iringa, laini za umeme Geita, Hoteli ya Johari Rotana, majengo ya Victoria Nobel na Peninsula Noble, na Uwanja wa Arusha unaojengwa kwa ajili ya AFCON mwakani.
Alisisitiza kuwa Watanzania wanachukua zaidi ya asilimia 90 ya wafanyakazi kwenye miradi ya CRJE kupitia mafunzo ya uanagenzi na Programu ya Kukuza Vipaji ya Ufundi wa Kichina, huku kampuni ikizingatia ujenzi wa kijani kama Kiwanda cha Mboji Kinondoni cha tani 50 kwa siku na teknolojia za kidijitali.







Social Plugin