Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHATANDA: CCM NDICHO CHAMA CHENYE KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI, TWENDENI TUKAMPIGIE KURA DKT. NETTHO NDILITO




Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 19 Oktoba 2026, amezungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi kutoka makundi mbalimbali katika mkutano wa ndani uliofanyika Kitongoji cha Chichinka, Kata ya Segala, Jimbo la Chamwino, Mkoani Dodoma, akisisitiza kuwa CCM ndicho chama chenye uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo na kuwataka kutowasikiliza matapeli wa kisiasa


Aidha, Chatanda amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi, tarehe 4, na kumpigia kura mgombea wa ubunge kupitia CCM, Dkt. Nettho Ndijina Ndilito, ili kukipa Chama Cha Mapinduzi ushindi wa kishindo na kukiheshimisha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com