Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NEEMA NKUMBI ATWAA TUZO YA BEST FEMALE MEDIA PERSONALITY MDAU SHUPAVU AWARDS 2026

Mwandishi wa habari Neema Nkumbi kutoka Wilayani Kahama ameibuka mshindi wa tuzo ya Mwanahabari Bora wa Kike 'Best Female Media Personality' katika tuzo za MDAU SHUPAVU Awards – Shinyanga 2026, Season 2, zilizotolewa Oktoba 20, 2026, katika ukumbi wa Miligo Hall, mjini Kahama, mkoani Shinyanga.

Neema ni miongoni mwa waandishi wa habari wanaotumia majukwaa mbalimbali ya kidijitali kufikisha habari na taarifa kwa jamii, akiandika kwa majukwaa yakiwemo Huheso Digital, Meza ya Mafanikio, Udadisi Live na Malunde 1 Blog.

Ushindi huo ni utambuzi wa mchango wake katika tasnia ya habari na nafasi ya wanawake katika kuhabarisha umma kupitia majukwaa ya kidijitali, ambayo yameendelea kuwa sehemu muhimu ya upashanaji habari na uelimishaji wa jamii.

Tuzo za MDAU SHUPAVU Awards zimeandaliwa na Taasisi ya HOLYSMILE, chini ya Mkurugenzi wake Arnold A. Bweichum Jr, kwa lengo la kutambua na kuenzi watu binafsi, taasisi na biashara zinazochangia maendeleo ya jamii katika sekta mbalimbali.

Tuzo hizo zimejumuisha kategoria mbalimbali zinazohusisha habari, biashara, ujasiriamali, burudani, elimu, mitindo na urembo, ubunifu na maendeleo ya jamii, huku washindi wakipatikana kupitia kura za wazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com