Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

OUTSO YAFANYA MKUTANO WA 45 SHINYANGA, WANAFUNZI ZAIDI YA 150 WALIPIWA ADA

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Josiah Zephania Katani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026. Picha na Kadama Malunde
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Josiah Zephania Katani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026. 

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUTSO), Felix Rugeyamu, akizungumza wakati wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUTSO) imefanya Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi mjini Shinyanga, ukijadili masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wa wanafunzi, huku uchaguzi mkuu wa viongozi wapya wa serikali hiyo ukitarajiwa kufanyika Oktoba 16, 2026.

Mkutano huo wa siku tatu ulioanza Oktoba 14 na kuhitimishwa Oktoba 16, 2026, umewakutanisha wawakilishi wa wanafunzi kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu wanafunzi na mustakabali wa uongozi wa OUTSO.

Miongoni mwa ajenda muhimu za mkutano huo ni uchaguzi wa viongozi wapya watakaosimamia serikali hiyo, wakiwamo Rais, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu.

Akizungumza katika mkutano huo leo, Oktoba 15, 2026, Rais wa OUTSO anayemaliza muda wake, Felix Rugeyamu, amesema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake, serikali hiyo imefanikiwa kuwalipia ada za masomo wanafunzi zaidi ya 150 waliokuwa na changamoto za kifedha, ili kuwawezesha kuendelea na masomo na kukamilisha safari yao ya kitaaluma.

“Tamaduni zetu za Kitanzania na katika vyuo vyetu, ni nadra kusikia Serikali ya Wanafunzi imewalipia wanafunzi wenzao ada ili waweze kuhitimisha masomo yao. Tumefanya hivyo kwa sababu Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ni tofauti na vyuo vingine vyote,” amesema Felix.
Felix Rugeyamu.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za uongozi wake katika kutetea maslahi ya wanafunzi na kuhakikisha changamoto za kifedha hazizuii wanafunzi kupata fursa ya kuendelea na masomo yao.

Akizungumzia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kesho, Felix amewataka viongozi watakaopatikana kuongoza kwa hekima, ukomavu na kuzingatia maslahi mapana ya wanafunzi.

Amewasisitiza kutumia majadiliano yenye kujenga katika kuwasilisha changamoto na hoja za wanafunzi, huku wakiheshimu taratibu zilizowekwa na kudumisha mahusiano mazuri na menejimenti ya chuo.

Amesema ni muhimu serikali ya wanafunzi kuendelea kuwa chombo kinachotafuta ufumbuzi wa changamoto za wanafunzi na kuimarisha ushirikiano, badala ya kuongozwa na mihemko katika kushughulikia masuala yanayohitaji majadiliano.

Kwa upande wake, mgeni rasmi katika mkutano huo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Josiah Zephania Katani, aliyemwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Alex Makulilo, amesema viongozi wa wanafunzi wana wajibu wa kuwa kiungo muhimu kati ya wanafunzi na menejimenti ya chuo.
Prof. Josiah Zephania Katani

Prof. Katani amesema uhusiano mzuri kati ya pande hizo unaweza kuimarishwa kupitia majadiliano yenye tija, kuheshimiana na kufuata taratibu zilizowekwa katika kushughulikia changamoto zinazowakabili wanafunzi.

Aidha, amewataka viongozi watakaochaguliwa kutambua kuwa wanapokuwa wajumbe wa baraza, wanakuwa na wajibu wa kushiriki katika maamuzi ya pamoja yanayozingatia maslahi ya wanafunzi, chuo na taifa kwa ujumla.

Amesisitiza kuwa baraza hilo linapaswa kuwa jukwaa la kujenga hoja, kubadilishana mawazo na kufikia maamuzi yenye manufaa, badala ya kuwa chombo cha kushindana na uongozi wa chuo.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika mkutano huo, akiwamo Caroline Robson, wamepongeza uongozi wa OUTSO unaomaliza muda wake kwa kuzingatia mahitaji ya wanafunzi, hususan wale waliokuwa na changamoto za kifedha.
Wamesema hatua ya kuwalipia ada wanafunzi wenzao inaonesha umuhimu wa serikali ya wanafunzi kuweka mbele maslahi ya wanachama wake na kushughulikia changamoto zao kwa vitendo.

Wametoa wito kwa viongozi watakaochaguliwa kuendeleza jitihada hizo, kuimarisha umoja miongoni mwa wanafunzi na kuhakikisha changamoto zinazowakabili zinapatiwa ufumbuzi kupitia mifumo na taratibu za chuo.

Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO unatarajiwa kuhitimishwa kesho, Oktoba 16, 2026, kwa uchaguzi mkuu wa viongozi wapya watakaokuwa na jukumu la kuendeleza uwakilishi wa wanafunzi na kusimamia masuala yanayohusu ustawi na maendeleo yao katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Josiah Zephania Katani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026. 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Josiah Zephania Katani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026. 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Josiah Zephania Katani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026. 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Josiah Zephania Katani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026. 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Josiah Zephania Katani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026. 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Josiah Zephania Katani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026. 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Josiah Zephania Katani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026. 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Josiah Zephania Katani, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi wa OUTSO mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026. 

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUTSO), Felix Rugeyamu, akizungumza wakati wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUTSO), Felix Rugeyamu, akizungumza wakati wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUTSO), Felix Rugeyamu, akizungumza wakati wa Mkutano wa 45 wa Bunge la Wanafunzi mjini Shinyanga, Oktoba 15, 2026.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com