Na Marco Maduhu, Elizabeth Cosmas, SHINYANGA
Wananchi wa Kijiji cha Mwanono Kata ya Didia wilayani Shinyanga, wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, kwa ahadi ya kuwapatia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho, ambayo imechukua muda mrefu kukamilika, na kusababisha kukosa huduma za afya karibu na makazi yao.
TAZAMA VIDEO👇👇
Wamebainisha hayo leo, Septemba 25, 2026, katika mkutano wa hadhara wa Mbunge Azza, uliofanyika kwa ajili ya kutoa shukrani, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mmoja wa wananchi hao Grace Mathias, amesema wanamshukuru Mbunge huyo kwa ahadi ya kuwapatia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo, ili kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kwenda Hospitali Binafsi ya Bugisi.
Mwananchi mwingine Asteria Kitindi, amesema wanamshukuru Mbunge huyo kwa ahadi hiyo ya kuwapatia mifuko hiyo ya saruji ili kukamilisha zahanati yao, ambayo itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi kupata huduma za matibabu kwa ukaribu, hasa wajawazito.
Naye Diwani wa Didia Richard Luhende, amempongeza Mbunge Azza kwa jitihada zake za kupigania maslahi ya wananchi, ikiwamo kuwasemea Bungeni, na kusaidia kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Mbunge wetu kafika tu hapa kwenye mkutano, akaona jengo letu la zahanati, akaumia, akasema, kumbe hapa kuna jengo kubwa, twendeni mkanionyeshe, tukamzungusha, akaliona na akaahidi kutoa mifuko 100 ya saruji, tunataka wabunge wa namna hii wenye uchu na changamoto za watu,” amesema Luhende.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, amesema analifahamu jengo hilo la zahanati, ambalo lina zaidi ya miaka 10 tangu lilipoanza kujengwa, kabla hata hajawa Mbunge wa Jimbo hilo.
Amesema, baada ya kulikagua, amebainisha baadhi ya mapungufu na kutoa ushauri wa kufanyiwa marekebisho, huku akiahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi.
Katika hatua nyingine, ameelezea utekelezaji wa miundombinu ya barabara, madaraja, umeme ngazi ya vitongoji, miradi ya maji kutoka Ziwa Victoria, pamoja na ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo.
Mbunge Azza, ameendelea na ziara yake ya kijiji kwa kijiji, ambapo leo alikuwa katika Kijiji cha Mwanono Kata ya Didia, na Kijiji cha Zobogo Kata ya Itwangi.
TAZAMA PICHA 👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Diwani wa Didia Richard Luhende akizungumza.
Diwani wa Itwangi Liyda Pius akizungumza.































































Social Plugin