Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TCRS NA HALMASHAURI YA KISHAPU WAFIKISHA ELIMU YA EL NINO KWA WANANCHI KATA YA TALAGA, WATAKIWA KUTOZUA TAHARUKI



Mratibu wa Maafa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga , Robert Mhina akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Kijiji cha Nendegese, Kata ya Talaga wilayani Kishapu kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño Septemba 25, 2026

Na Sumai Salum-Kishapu

WANANCHI wa Kijiji cha Nendegese, Kata ya Talaga, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, wametakiwa kutotengeneza taharuki wakati wa kipindi cha mvua za El Niño, badala yake kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa sahihi za hali ya hewa kutoka vyanzo rasmi.


Hayo yamesemwa leo Septemba 25, 2026, kwenye mkutano wa hadhara wa kijiji na Mratibu wa Maafa Wilaya ya Kishapu, Robert Mhina, wakati akitoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujiandaa na kujikinga dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo zoezi lililoratibiwa na Shirika la Tanganyika Christian Refugee Services (TCRS) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa ufadhili wa shirika la Norwegian Church Aid (NCA) .


“Wananchi tunawasihi kutotengeneza taharuki wala kusambaza taarifa zisizo sahihi kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye makazi yenu wakati wa kipindi hiki cha mvua. Muhimu ni kufuatilia taarifa kutoka vyanzo rasmi, kuchukua tahadhari mapema na kuhakikisha familia, watoto, mifugo na mali zinalindwa,” amesema Mhina.


Amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na maeneo hatarishi wakati wa mvua, ikiwemo maeneo ya mabonde, mito na vivuko, huku akiwataka wazazi na walezi kuhakikisha usalama wa watoto na kuchukua tahadhari wakati wa kuvuka maeneo yenye maji.

Kwa upande wake, Mwezeshaji kutoka Shirika la Tanganyika Christian Refugee Services (TCRS) mkoani humo, Raiya Milonga, amesema shirika hilo linaendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha uelewa na uwezo wa jamii kukabiliana na majanga, ikiwemo kupitia elimu ya maandalizi, kinga na mwitikio wa majanga pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

“TCRS inaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha jamii inakuwa salama na yenye uwezo wa kukabiliana na majanga. Tunatoa elimu, tunajenga uwezo wa wananchi na pia tunaweka msisitizo katika kuwawezesha kiuchumi ili waweze kujikwamua na kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali,” amesema Raiya.

Wananchi pia wamepewa elimu kuhusu utunzaji wa mazingira, usafi wa mazingira, matumizi salama ya maeneo ya makazi pamoja na umuhimu wa kufuatilia taarifa za hali ya hewa na kuzitumia katika kufanya maamuzi sahihi.


Baadhi ya wananchi waliopewa elimu hiyo akiwemo Debora Jacobo na Singili Masali Singili wamepongeza hatua hiyo, wakisema imewasaidia kuelewa namna ya kulinda usalama wa watoto, hasa wakati wa kuwapeleka au kuwatoa mifugo malishoni katika kipindi cha mvua.


Aidha, wameiomba Serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya vivuko katika maeneo muhimu, ikiwemo kivuko cha daraja kinachounganisha Kijiji cha Nhobola na Nendegese pamoja na kivuko kinachoelekea Shule Shikizi ya Nendegese, ili kupunguza hatari kwa wananchi wakati wa mvua.


Kwa ujumla, Shirika la Tanganyika Christian Refugee Services (TCRS) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kwa ufadhili wa shirika la Norwegian Church Aid (NCA)_ limeendelea imeendelea kuonesha juhudi katika kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya majanga kwa kuelimisha jamii, kuimarisha uwezo wa wananchi wa kukabiliana na athari za majanga, kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kuwawezesha wananchi kiuchumi ili waweze kujikwamua na kujenga jamii yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Mwezeshaji kutoka Shirika la Tanganyika Christian Refugee Services (TCRS) mkoani humo, Raiya Milonga akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Kijiji cha Nendegese, Kata ya Talaga wilayani Kishapu kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño Septemba 25, 2026Mratibu wa Hali ya Hewa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Deus Gomba, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Kijiji cha Nendegese, Kata ya Talaga wilayani Kishapu kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño Septemba 25, 2026
Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Charles Kanwakabo akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Kijiji cha Nendegese, Kata ya Talaga wilayani Kishapu kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño Septemba 25, 2026
Kaimu mwenyekiti wa kijiji cha Nendegese Kata ya Talaga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Saidi Kija kademe akizungumza kwenye mkutano huo

Mtendaji wa Kijiji cha Nendegese Kata ya Talaga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Rosemary Msengi Gunda akizungumza kwenye mkutano huo
Mkazi wa Kijiji cha Nendegese Kata ya Talaga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Debora Jacobo
Mkazi wa Kijiji cha Nendegese Kata ya Talaga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Singili Masali SingiliKivuko kinachoelekea Shule Shikizi ya Nendegese Kata ya Talaga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga
Eneo la kunyweshea mifugo Kijiji cha Nendegese Kata ya Talaga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga





























Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com