Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANGA UWASA YAIBUKA KINARA C_CEOs FORUM 2026





Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) imeibuka mshindi wa kwanza na kutunukiwa Tuzo katika kipengele cha Shirika la Umma la Kibiashara lililofanya vizuri zaidi katika Menejimenti ya Rasilimali-Fedha, kupunguza matumizi na kuongeza ufanisi katika urejeshaji wa Mtaji

Tuzo hiyo imetolewa leo wakati wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum 2026), kilichofanyika katika Ukumbi wa Arusha International Conference Centre (AICC), Arusha.


Makamu wa Rais, Mhe. Deo Ndejembi, ametoa pongezi kwa Tanga UWASA kwa kutambuliwa kwa utendaji wake, akisisitiza umuhimu wa Taasisi na Mashirika ya Umma kuendelea kuimarisha usimamizi wa rasilimali, kuongeza ufanisi na kuhakikisha yanatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.

Mafanikio hayo yanaendelea kuonesha umuhimu wa usimamizi bora wa rasilimali katika Taasisi na Mashirika ya Umma, hususan katika kuimarisha ufanisi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com