Na Mwandishi Wetu, Dar esalaam
Kuelekea maadhimisho ya siku ya moyo duniani, Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wanatarajia kutoa huduma za vipimo vya magonjwa ya moyo bila malipo kwa abiria wote wataosafiri na treni ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge, amesema kuwa huduma hiyo ya vipimo vya afya na uchunguzi wa magonjwa ya moyo na yake yasiyoambukiza itaanza kuanzia septembea 21 hadi 27 ikiwa ni wiki maalum kupelekea kileleni cha siku ya moyo itakayoadhimishwa septemba 29,2026
Amesema wataalamu na mabingwa wa afya watakuwa wakisafiri ndani ya treni ya SGR ili kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo na mengine yasiyo ya kuambukiza kwa abiria wote watakaopenda kupimwa.
"Vipimo hivi vyote vikiwemo Echo, ECG, vipimo vya sukari na mafuta kwenye damu vikitolewa hospitalini vinaweza kugharimu zaidi ya Shilingi 500,000, lakini kwa kipindi hiki chote cha wiki ya afya ya moyo, abiria wote watapata huduma hizi bure kabisa wakiwa safarini," amesema Dkt. Kisenge.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la reli Tanzania (TRC)Mhandisi Masanja Machibya, ameeleza kuwa ushirikiano huo ni mwanzo wa mpango mkubwa zaidi wa kimkakati kwa shirika hilo katika kuhakikisha abiria wake wanapata huduma za afya wakiwa ndani ya treni ya kisasa ya SGR.
Ameongeza kuwa,TRC ipo kwenye hatua za usanifu za kutengeneza mabehewa maalum yatakayokuwa na vifaa vya matibabu na vitanda (ambualansi ya treni) ili kuwasafirisha wagonjwa mahututi na wanaopewa rufaa kutoka mikoani kuja Mharimbili au hospitali kuu kwa haraka na usalama zaidi.
"Mabehewa haya yatasaidia sana kupunguza muda wa kusafirisha wagonjwa waliopo kwenye hali mbaya kutoka mikoani kama Dodoma na Morogoro kulinganisha na kutumia magari ya dharura (ambulance) ya barabarani. Mpango huu wa mabehewa ya matibabu unatarajiwa kuanza kufanya kazi ndani ya miezi sita ijayo," aliongeza Mhandisi Machibya.
Viongozi hao wametoa wito kwa wananchi na abiria wote wanaosafiri na SGR katika wiki hiyo kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo kupima na kuchunguza afya zao.

Social Plugin