Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BODABODA ITILIMA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI WA EL NINO


Na Sumai Salum-Kishapu


MKUU wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amewataka wananchi wa Vijiji vya Mwamala “A” na Nalindilo, Kata ya Itilima, kuchukua tahadhari mapema dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua, hususan wanaoishi katika maeneo ya mabondeni na karibu na mikondo ya maj


Mhe. Masindi ametoa wito huo leo Septemba 29, 2026, alipofanya ziara katika Vijiji hivyo na kufanya mkutano wa hadhara kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi, kutoa elimu pamoja na kuwahamasisha kuchukua hatua za mapema kulinda maisha, familia na mali zao.


Amesema Serikali haijasubiri mvua kubwa kuanza ndipo itoe elimu, bali imeanza maandalizi mapema ili wananchi wawe tayari kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza, akisisitiza kuwa jambo la msingi si kusubiri mvua nyingi, bali kuwa na maandalizi na uwezo wa kukabiliana na athari zake.


“Tusisubiri maji yafike ndipo tuanze kuchukua hatua. Wanaishi maeneo ya mabondeni na karibu na mikondo ya maji waanze kutafuta maeneo salama mapema, watoto wapelekwe na kufuatwa mashuleni na pia waendapo popote waende kwa makundi makundi na nyie bodaboda hakikisheni mnachukua tahadhari ya kuvuka maeneo yenye maji hatutaki kusikia uzembe unapelekea kuhatarish” amesema Mhe. Masindi.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed, amewataka wananchi kutosubiri athari ziwafikie, bali waanze maandalizi mapema, ikiwemo kuhamia maeneo salama wale wanaoishi katika maeneo hatarishi. Aidha, amewataka wananchi kwa dini zao kuendelea kumuomba Mungu ashushe mvua za kiasi huku wakichukua tahadhari zinazostahili.


Katika mkutano huo, wananchi waliwasilisha changamoto mbalimbali zikiwemo barabara kutopitika wakati wa mvua, vivuko hatarishi kwa wanafunzi, upungufu wa nyumba za walimu pamoja na hitaji la madaraja katika maeneo mbalimbali huku wakiiomba Serikali kuweka mazingira salama kwa watoto wanaovuka maeneo hatarishi wanapokwenda shule.


"Leo tumekaa na Watendaji wa Kata na serikali imetoa maelekezo ya kuhakikisha wanawatambua wananchi kila mmoja mwenye mazao yake na kisha kuandaa kwa kushirikisha jamii kuenga eneo ambalo ni salama kwa uhifadhi wake" ameongeza Fatma


Kuhusu changamoto za barabara na madaraja, TARURA imewataka wananchi kushirikiana katika kulinda miundombinu ya barabara, madaraja na makaravati kwa kuepuka kuweka vizuizi vinavyoweza kuzuia mtiririko wa maji.


Pia imeeleza kuwa katika eneo la Daraja la Ikoma kwenye Mto Mumbu, kuna jitihada za kutengeneza kipande cha takribani kilomita moja ili wananchi waweze kupata njia ya kupita, kweni ujenzi wa daraja hilo unahitaji zaidi ya Sh. milioni 700.


Katika sekta ya kilimo, Afisa Kilimo na Mratibu wa Zao la Pamba, Richard Mangua, amewataka wananchi kuweka usalama wao na familia zao mbele, huku wakijiandaa na msimu wa kilimo kwa kufanya usafi wa mashamba ya pamba na kulima mazao yanayofaa katika maeneo yao na yanayostahimili unyevu mwingi ikiwa ni pamoja na mpunga, viazi vitamu na mtama.


Mangua pia amewataka wakulima kutumia mbegu na pembejeo bora pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya ndege waharibifu wa mazao, huku akieleza kuwa mbegu za pamba zitaanza kuletwa wiki mbili za mwanzo za mwezi Oktoba.


Kuhusu elimu, wananchi wameeleza changamoto ya upungufu wa vyoo Shule ya Msingi Ipillilo, ambapo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamala "a" Masalu Jidalika Shimbi amesema ujenzi wa vyoo hivyo umeanza kwa kushirikisha Sungusungu na nguvu za wananchi, ukiwa na thamani ya takribani Sh milioni 5 na ofisi ya Jimbo.


"Mhe. mkuu wetu wa Wilaya kwanza nikupongeze sana kwa jitihada na moyo wa kuja kututembelea sisi wana Mwamala na Nalindilo, pili nikuoombe mtusaidie ujenzi wa nyumba za kuishi walimu huku kwani hazitoshi jambo linalopelekea walimu kukaa mbali na vituo vyao vya kazi" amesema Salome Eliud


Wananchi hao wametakiwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu muhimu ya kijamii ikiwemo shule, zahanati na huduma nyingine, akisisitiza kuwa maendeleo ya Vijiji yanahitaji ushirikiano wa Serikali, Wadau na Wananchi.


Aidha viongozi wa vijiji wametakiwa kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika shughuli za maendeleo ili wajione kuwa sehemu ya maeneo yao, huku akisisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari mapema badala ya kusubiri majanga yatokee ndipo hatua zichukuliwe.Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Vijiji vya Mwamala "A" na Nalindilo Kata ya Itilima wilayani humo Septemba 29,2026

Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi na wananchi wa Vijiji vya Mwamala "A" na Nalindilo Kata ya Itilima wilayani humo Septemba 29,2026
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe Peter MasindiKatibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed

Afisa Kilimo na Mratibu wa zao la pamba Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Richard Mangua
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Nalindilo Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Dotto Thomas

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mwamala "A" Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Masalu Jidalika Shimbi

Afisa Kilimo na Mratibu wa zao la pamba Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Richard Mangua akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Peter Masindi na wananchi wa Vijiji vya Mwamala "A" na Nalindilo Kata ya Itilima wilayani humo Septemba 29,2026

Mwakilishi wa Mhandisi wa Tarura wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akijibu maswali

Mkazi wa Kijiji Cha Mwamala "A" Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Salome Eliud akizungumza
Mkazi wa Kijiji cha Nalindilo Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Veronica Masanja akizungumza
Tungu Jidaleka akizungumza
Punguja Kabh'elele akizungumza
Salum Nyarobi Akizungumza

Mkazi wa Kijiji Cha Mwamala "A Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Maganga Shija akizungumza



















































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com