NA NEEMA NKUMBI, KAHAMA
Nabii Nicolaus Suguye ameahidi kutoa matofali 3,000 pamoja na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika Kituo cha Kahama Peace Orphanage Center, kilichopo Mtaa wa Dodoma Viwandani, Kata ya Zongomela, Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Ahadi hiyo ameitoa Septemba 8, 2026, alipotembelea kituo hicho baada ya uongozi wa kituo kueleza changamoto ya ukosefu wa uzio, hali ambayo imekuwa ikihatarisha usalama wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Nabii Suguye amesema jamii ina wajibu wa kushirikiana katika kuwasaidia watoto wenye uhitaji, akisisitiza kuwa msaada kwa watoto hao haupaswi kuishia kwenye chakula pekee, bali unapaswa kujumuisha mahitaji mengine muhimu yanayoweza kuboresha maisha na mustakabali wao.
Amesema kushirikiana katika kutatua changamoto zinazovikabili vituo vya kulelea watoto ni sehemu ya wajibu wa jamii, kwani mazingira bora yana nafasi kubwa katika malezi na maendeleo ya watoto.
Mkurugenzi wa Kahama Peace Orphanage Center, Abubakari Issa, amesema ukosefu wa uzio ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili taasisi hiyo, kwani baadhi ya watoto wamekuwa wakitoka nje ya eneo la kituo na kukutana na mazingira yanayoweza kuhatarisha usalama wao.
Issa amesema kituo hicho tayari kimeanza ujenzi wa msingi wa uzio, lakini kimekuwa kikikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi vinavyohitajika ili kukamilisha kazi hiyo.
“Watoto wetu wamekuwa wakipotea na kukutana na mambo yanayohatarisha usalama wao, kama kung’atwa na mbwa, kutokana na ukosefu wa uzio. Lakini kwa sababu Nabii Suguye amekuja na kuelewa changamoto yetu, sina shaka kwamba atatusaidia,” amesema Issa.
Amesema kukamilika kwa ujenzi wa uzio kutasaidia kuimarisha usalama wa watoto na kuiwezesha kituo hicho kuendelea kutoa malezi katika mazingira salama, hususan kwa kuwa kinapokea watoto wadogo, wakiwemo walio chini ya umri wa miaka mitano.
Mbali na Kahama Peace Orphanage Center, Nabii Suguye pia ametembelea Kituo cha New Hope Orphanage Center, kilichopo Mtaa wa Mwime, Kata ya Zongomela, ambako ametoa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Miongoni mwa mahitaji yaliyotolewa ni sukari, maharage, sabuni, mafuta ya kupikia, unga wa sembe pamoja na mahitaji mengine ya matumizi ya kila siku.
Akizungumza kuhusu kituo hicho, Msimamizi wa New Hope Orphanage Center, Scolastika Fred, amesema taasisi hiyo inatoa malezi pamoja na elimu kwa watoto wenye uhitaji, kuanzia shule ya msingi hadi ngazi ya chuo kikuu.
“Tuna kituo kinachotoa malezi pamoja na elimu kwa watoto wenye uhitaji wa kusoma, kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu. Tunashukuru sana kwa ujio wenu. Tunaomba Mungu awabariki na awaongezee kila siku,” amesema Scolastika.
Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho, Judith Suleman, amemshukuru Nabii Suguye kwa msaada huo, akisema jamii ina nafasi kubwa katika kuwasaidia watoto wenye uhitaji.
Amesema licha ya changamoto wanazokutana nazo, baadhi ya watu wamekuwa wakijitolea kuwasaidia, jambo ambalo amesema ni sehemu ya mshikamano na upendo wa jamii.
“Tunawashukuru sana. Hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuwaambia tunawashukuru. Mungu ambariki kila anayejitolea kutusaidia,” amesema Judith.
Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya shughuli za Nabii Suguye katika Manispaa ya Kahama, kabla ya kuanza kwa mkutano wa injili unaotarajiwa kuanza Septemba 9, 2026.

Social Plugin