Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PROF. SHEMDOE ATUMA SALAMU ZA POLE KIFO CHA MAMA FATUMA KARUME


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, anaungana na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa salamu za pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi; Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume, pamoja na wanafamilia, ndugu, jamaa na Wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote, kufuatia kifo cha Mama Fatuma Karume, mke wa Hayati Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Mama Fatuma Karume amefariki dunia tarehe 21 Septemba 2026, Zanzibar.

Mhe. Prof. Shemdoe anaungana na familia, ndugu, jamaa na wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote katika kipindi hiki cha majonzi, huku akiomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi na kuwapa wafiwa nguvu, subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Apumzike kwa amani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com