Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI KAPINGA AAGIZA MIRADI YOTE YA MAENDELEO KUKAMILIKA KWA WAKATI


Serikali imetoa agizo kwa wakandarasi na wasimamizi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Masasi kuhakikisha miradi yote inakamilika ndani ya muda uliopangwa, na kusisitiza kuwa utamaduni wa kuongeza muda wa utekelezaji (extension) hauleti tija wala maendeleo kwa Taifa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb), wakati akikagua na kuzindua ghala la kuhifadhia mazao Agosti 10, 2026 katika kata ya Mtandi, Halmashauri ya Mji wa Masasi linalojengwa na Halmashauri hiyo na kutaka kila mkandarasi kuongeza nguvu kazi na kasi ya utendaji kazi ili miradi ikamilike kwa haraka na kuwa yenye tija na ubora wa huduma unategemea sana utekelezaji wa haraka na uwekezaji katika mnyororo mzima wa uhifadhi wa bidhaa.

Aidha, ametoa rai ya kuongeza kasi kwenye zao la korosho, akieleza kuwa korosho ni biashara Kuu ya eneo hilo na isipopewa msukumo wa haraka, Mji wa Masasi na Taifa kwa ujumla havitapata mapato yanayotarajiwa.

Vilevile, ameeleza kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kuibeba na kuiwezesha Sekta Binafsi kwa kiwango sawa na Sekta ya Umma, ikilenga kuhakikisha asilimia 70 ya mitaji ya maendeleo inatoka katika sekta hiyo binafsi kupitia mikakati kabambe iliyowekwa na Wizara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com