Na Sheila Ahmadi, Dodoma
Serikali imesema inaendelea kuweka na kuboresha sera pamoja na sheria zinazohusu usimamizi wa rasilimali za maji, kwa lengo la kuhakikisha kuwa rasilimali hiyo inalindwa na kutumika kwa tija kwa manufaa ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Afisa progaramu kutoka Shahidi wa maji John Emmanuel ambapo amesema kuwa kwenye sekta ya maji ni msingi muhimu katika kuongeza tija kwenye kilimo, maendeleo ya viwanda na ustawi wa jamii nchini.
wadau wametakiwa kuhakikisha shughuli za uzalishaji zinafanyika kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira, hususan maeneo ya vyanzo vya maji, ili kuepusha athari zinazoweza kuhatarisha upatikanaji wa maji kwa kizazi cha sasa na kijacho.
“Uhakika wa maji ni usalama wa taifa. Hii ndiyo imani yetu, kwa sababu bila maji hatuwezi kuendelea na kilimo, na bila maji ya uhakika hatuwezi kuwa na viwanda,” imeelezwa.
Wadau wa sekta hiyo pia wametakiwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha rasilimali za maji zinalindwa na kutumika kwa ufanisi, kwa kuwa jukumu hilo haliwezi kufanywa na taasisi moja pekee.
Aidha, kila mdau, ikiwemo Serikali, kampuni binafsi na taasisi zinazojihusisha na shughuli za uzalishaji, anapaswa kuzingatia upatikanaji wa maji ya uhakika wakati wa kupanga na kutekeleza shughuli zake.
Hata hivyo ushirikiano wa wadau ni muhimu katika kuhakikisha rasilimali za maji zinakuwa endelevu na zinachangia kufikia malengo ya maendeleo ya taifa, ikiwemo kuongeza uzalishaji wa chakula na kukuza sekta ya viwanda.

Social Plugin