Na Sumai Salum – Kishapu
Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo la kujadili taarifa za robo ya nne mwaka wa fedha 2025/2026 Agosti 5,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Fatma Mohamed, amewataka Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuendelea kuwa mabalozi wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuvuna, kuhifadhi na kusafirisha pamba kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa ili kulinda ubora wa zao hilo.
Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu uliokuwa ukijadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026, Fatma amesema Madiwani wana nafasi kubwa ya kuhakikisha elimu hiyo inawafikia wananchi katika kata zao ili kuongeza tija ya kilimo cha pamba.
Amesema uhifadhi sahihi wa pamba hupunguza upotevu wa mazao, huongeza thamani ya pamba katika soko, huwapa wakulima fursa ya kupata bei nzuri na kuimarisha mchango wa zao hilo katika ukuaji wa uchumi wa Wilaya ya Kishapu na Taifa kwa ujumla. Aidha, amewasisitiza kuendelea kushirikiana na wataalamu wa kilimo na wadau mbalimbali katika kuhamasisha uzalishaji wa pamba yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko la ndani na la kimataifa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo la kujadili taarifa za robo ya nne mwaka wa fedha 2025/2026 Agosti 5,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Josephat Limbe, amesema madiwani wanapaswa kuendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika kwa uadilifu na kwa manufaa ya wananchi. Amesema usimamizi madhubuti wa miradi, uwajibikaji na ushirikiano kati ya viongozi na wananchi ni msingi wa kuharakisha maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma katika sekta zote muhimu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Emmanuel Johnson, amesema Serikali inaendelea kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika ukusanyaji wa mapato na utoaji wa huduma ili kuondoa mianya ya ubadhirifu na kuongeza uwazi. Amesema Serikali imejidhatiti kuachana na malipo ya fedha taslimu katika huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulipaji wa fedha za pamba na kuelekeza matumizi ya malipo ya kielektroniki, hatua inayorahisisha ufuatiliaji wa mapato, kuongeza uwajibikaji na kulinda fedha za umma.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo la kujadili taarifa za robo ya nne mwaka wa fedha 2025/2026 Agosti 5,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Pamba Tanzania ambaye pia ni mkaguzi wa pamba wilayani humo Joachimu Gobanya amesema wajibu wa bodi ya pamba Tanzania ni kuhakikisha wanaendelea kuelimisha wakulima kuzingatia kanuni bora za uzalishaji, uvunaji na uhifadhi wa pamba ili kuongeza ubora wa zao hilo na kulifanya liwe na ushindani zaidi katika soko. Amesema pamba yenye ubora ni chachu ya kuongeza kipato cha mkulima na kukuza uchumi wa Taifa.
Gobanya ameongeza kuwa bodi hiyo inaendela kusiamamia sheria, kanuni na miongozo ya ununuzi wa pamba ikiwa ni pamoja na kuhakikisha pamba inayonunuliwa kupitia Vyama vya Msingi vya Ushikia AMCOS ni safi na yenye ubora ambapo kwa Wilaya ya kishapu kuna jumla ya AMCOS 74 mpaka sasa zizlizopigwa faini kwa makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na usimamizi duni wa ubora na usafi wa pamba ni 18.

Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Adonias Nyamjulirwa, akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la madiwani wilayani Kishapu mkoani humo wa kujadili taarifa mbalimbali za robo ya nne mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika Agosti 5, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Kwa upande wa sekta ya madini, Mwakilishi wa Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga Seleman Shamlugu, amesisitiza umuhimu wa wananchi kuendesha shughuli za uchimbaji kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa pamoja na kulinda mazingira. Amesema sekta ya madini inaendelea kuwa kichocheo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi, hivyo ushirikiano wa viongozi na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha rasilimali hizo zinaleta manufaa kwa jamii na Taifa.
Akizungumza wakati akijibu maswali ya Waheshimiwa Madiwani kuhusu idadi ya leseni za madini wilayani humo na namna Halmashauri itanufaika, ambapo amesema kuna jumla ya leseni 162 ikiwa ni pamoja na Leseni 76 za Almasi, 80 Dhahabu na 6 za Ujenzi amesema tayari wameweka mipango ya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ili kuhakikisha inanufaika kupitia tozo za huduma.
Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ulianza jana kwa kupokea na kujadili taarifa za maendeleo kutoka katika Kata mbalimbali, kabla ya kuhitimishwa leo kwa kujadili taarifa za utekelezaji wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na taarifa za Kamati za Kudumu za Baraza, zikiwemo Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Kamati ya Elimu, Afya na Maji, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira pamoja na Kamati ya Maadili. Mijadala hiyo imelenga kuimarisha uwajibikaji, kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma na kuharakisha maendeleo ya Wilaya ya Kishapu.
Mwakilishi wa Bodi ya Pamba Tanzania ambaye pia ni Mkaguzi wa pamba wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Joachimu Gobanya akijibu maswali ya Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwenye mkutano wa Baraza la madiwani la robo ya nne mwaka wa fedha 2025/2026 wenye lengo la kujadili taarifa za robo hiyo Agosti 5, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri

Mwakilishi wa Afisa madini mkazi mkoani Shinyanga Seleman Shamlugu akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani humo wa kujadili taarifa za robo ya nne mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Agosti 5, 2026
Makamo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Enoch Reubeni akifuatilia mkutano wa baraza hilo

Social Plugin