Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akiwapakulia chakula wanafunzi wa Shule ya Sekondari Luhumbo baada ya kuwaandalia chakula cha mchana, Agosti 7, 2026. Picha na Kadama Malunde
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akila chakula cha pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Luhumbo baada ya kuwaandalia chakula cha mchana, Agosti 7, 2026.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akila chakula cha pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Luhumbo baada ya kuwaandalia chakula cha mchana, Agosti 7, 2026.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akilishwa chakula na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Luhumbo wakati wa chakula cha pamoja alichowaandalia wanafunzi hao, Agosti 7, 2026.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akipiga picha ya kumbukumbu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Luhumbo baada ya kuwaandalia na kushiriki nao chakula cha pamoja, Agosti 7, 2026.
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, amewaandalia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Luhumbo chakula cha pamoja na kushiriki kula nao, huku akiwahimiza kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao na kufanikisha malengo yao ya kielimu.
Azza ameshiriki chakula hicho leo Agosti 7, 2026, shuleni hapo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Amesema hivi karibuni alipofika shuleni alikuta wanafunzi wakipata chakula cha mchana, jambo lililomfurahisha baada ya kupokea taarifa kuwa shule zote katika Kata ya Didia zinatoa chakula kwa wanafunzi.
Kutokana na hali hiyo, aliamua kuwaandalia chakula cha pamoja na kula nao, kama sehemu ya kuwapa hamasa na kuonyesha mshikamano.
Mbunge huyo amewataka wanafunzi kutumia vyema fursa ya mazingira bora ya kujifunzia yaliyowekwa na Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika masomo yao.
"Someni kwa bidii. Ninatarajia matokeo ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Luhumbo yatakuwa mazuri. Naahidi kwamba msichana mmoja na mvulana mmoja watakaopata Division One, nitagharamia mahitaji yote ya masomo yao ya awali watakapojiunga na Kidato cha Tano," amesema Azza.
Pia amewakumbusha wanafunzi kuthamini uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya elimu, ikiwemo ujenzi wa majengo mapya ya shule na madarasa yanayoendelea kujengwa katika Shule ya Sekondari Luhumbo.
Kwa upande wao, baadhi ya wanafunzi, akiwemo Riziki Paulo, wamemshukuru Mbunge huyo kwa kuwaandalia chakula cha pamoja, kula nao na kuwapa moyo wa kusoma kwa bidii, wakiahidi kuongeza juhudi katika masomo yao ili kufanya vizuri kwenye mitihani.
@malundeblog Mbunge wa Jimbo la Itwangi Mhe. Azza Hillal Hamad ameshiriki chakula cha pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Luhumbo iliyopo katika kata ya Didia katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Mbunge huyo ameandaa chakula hicho baada ya kutembelea shule hiyo
♬ original sound - Malunde blog



















Social Plugin