Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAONYESHO YA NANENANE YAMFUNGULIA MKULIMA NJIA YA SOKO lA NJE KIBIASHARA MKURUGENZI NEEMA




Na Sheila Ahmadi, Dodoma


mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni ya Grew inayopatikana mkoani Iringa, Neema Mwamoto, amesema safari ya kuanza kupitia kwenye kilimo haikuwa rahisi, huku mafunzo na ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali vimemsaidia kukuza uzalishaji na kuanza kulenga soko la nje.

Akizungumza na Wanahabari kwenye Maonyesho ya Nanenane jijini Dodoma Mkurugenzi wa Kampuni ya Groove Bi Neema Mwamoto Amesema kuwa Nilifanya Maamuzi ya kuingia kwenye kilimo baada ya kukutana na watu waliokuwa wakifanya shughuli hiyo kwa mafanikio, jambo ambalo lilinivutia na kumfanya nianze kilimo kwa vitendo Zaidi.

baada ya kuanza, aliamua kutosalia kwenye kilimo cha kawaida, bali kuongeza ujuzi na viwango vya uzalishaji ili aweze kufikia hatua ya kuuza mazao yake katika masoko ya kimataifa.

Akiendelea na safari hiyo, amesema alikutana na wadau mbalimbali waliomsaidia kupitia mafunzo ya kujenga uwezo, maarifa pamoja na kumtambulisha kwa wadau wengine waliokuwa tayari kumuunga mkono katika shughuli zake.

“Wamenisaidia sana kwenye capacity building, wamenikutanisha na wadau mbalimbali ambao ni wawezeshaji. Nimefika hapa naweza kusema najivunia, kwa sababu ni jitihada kubwa sana zilizofanywa na wamenisaidia kunijenga na kuniimarisha,” amesema Mwamoto".

Aidha Neema amesema ushiriki wake katika maonesho mbalimbali umekuwa fursa muhimu kwake kujifunza, kupata uzoefu na kutengeneza mtandao wa kibiashara pamoja na wadau wa sekta ya kilimo.

Kupitia maonesho hayo yamewapa nafasi wakulima na wajasiriamali wadogo kuonyesha bidhaa zao na kukutana na taasisi pamoja na washirika wa maendeleo wanaoweza kuwasaidia kukuza biashara zao.

Kufikia hadi sasa Neema amesema kampuni yake inalima aina mbili za mazao, huku akieleza kuwa bado wanahitaji kuongeza uzalishaji ili kufikia kiwango kinachoweza kukidhi mahitaji ya masoko ya nje.

Aidha katika kuongeza uzalishaji ni muhimu kwa kuwa soko la kimataifa linahitaji kiasi kikubwa cha mazao na uzalishaji mdogo unaweza kushindwa kukidhi mahitaji ya wanunuzi.

Nitoe Wito kwa vijana na watu wengine wanaotamani kuingia kwenye kilimo, Neema amewataka wasisite kuanza, akisisitiza umuhimu wa kupata taarifa sahihi na kujifunza kabla ya kuwekeza.

Katika hatua nyingine amesema kilimo kina fursa kubwa za kiuchumi endapo mkulima atakuwa na maarifa sahihi, atazingatia viwango vya ubora na kuwa na uwezo wa kuzalisha kwa kiwango kinachokidhi mahitaji ya soko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com