Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAONO YA RAIS SAMIA KUFANIKISHA MARIDHIANO, KATIBA

Tanzania imebarikiwa kuwa na kiongozi wa kipekee, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mwanamke mwenye moyo wa taifa, mwenye maono ya mbali, na asiyejikita katika maslahi yake binafsi, ambapo kupitia uongozi wake wananchi wanapaswa kukumbuka daima kwamba suala la mchakato wa katiba mpya lipo mikononi mwake na linaendelea kushughulikiwa kwa vitendo na si kwa maneno matupu. 

Katika historia ya Afrika, viongozi wengi wamekuwa wakishikilia madaraka kwa nguvu zaidi, wakiogopa mabadiliko yanayoweza kupunguza mamlaka yao, lakini Rais Samia ameonyesha sifa tofauti kabisa ya kujitolea kwa ajili ya taifa na si kwa ajili yake mwenyewe.

Kumbukumbu ya wananchi inapaswa kuonesha wazi kuwa hii ndiyo sababu iliyomfanya aone umuhimu wa katiba mpya, kwani katiba iliyopo imetumika kwa miongo mingi na wakati umefika wa kuifanyia marekebisho ili iendane na mahitaji ya kizazi cha sasa na kijacho. 

Rais Samia hakusubiri shinikizo la wapinzani wala kelele za mitaani, bali aliamua mwenyewe kwa hiari kuweka msingi thabiti wa mchakato huu muhimu, jambo ambalo si ishara ya udhaifu bali ni ishara ya ujasiri na upendo wa kweli kwa Tanzania.

Kupitia falsafa ya 4R yaani Maridhiano, Ustahimilivu, Marekebisho na Ujenzi Upya, wananchi wanakumbuka jinsi Rais Samia alivyosema na kutenda kwa kuanza kwa kuunganisha taifa, kuondoa marufuku ya mikutano ya hadhara, kupitisha sheria muhimu za uchaguzi zikiwepo Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Gharama za Uchaguzi, na Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi, pamoja na kutenga mabilioni ya shilingi kuimarisha vyama vya siasa. 

Hatua hizi zote ambazo wananchi wanazishuhudia na kuzikumbuka zilikuwa maandalizi ya kimkakati ili mchakato wa katiba mpya utakapoanza usiwe na vurugu, bali uwe wa amani, ushirikishwaji na heshima.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com