Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATIBU WA BUNGE ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI TENDAJI YA CPA KANDA YA AFRIKA



Katibu wa Bunge ambaye pia ni Katibu wa Kanda ya Afrika wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA Africa Region), Ndg. Baraka Leonard, ameshiriki Kikao cha Kamati Tendaji ya Chama hicho kilichofanyika leo, tarehe 11 Agosti 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu (BICC), Jijini Lilongwe, nchini Malawi.

Kikao hicho kimefanyika kabla ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa CPA Kanda ya Afrika unaotarajiwa kufanyika tarehe 14 Agosti 2026.

Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa CPA Kanda ya Afrika ambaye pia ni Spika wa Bunge la The Gambia, Mhe. Fabakary Jatta. Aidha, kikao hicho kimehudhuriwa na Mjumbe wa Mkutano huo kutoka Bunge la Tanzania, Mhe. Rose Tweve.

Mkutano Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola, Kanda ya Afrika, umeanza tarehe 10 Agosti 2026 na unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 16 Agosti 2026.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com