Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DG NEMC ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA–USIMAMIZI WA MAZINGIRA


-Ni katika hitimisho la Kongamano la FARViBE 2026,lililofanyika Jijini Dar es salaam

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.Immaculate Sware Semesi ametunukiwa tuzo ya heshima na Naibu Waziri Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu - Zanzibar, Mhe. Mboja Ramadhan Mshenga katika Kongamano la kimataifa la Kisayansi la Utafiti wa Uvuvi na Ufugaji wa Samaki kwa Uchumi wa Buluu Endelevu (FARViBE 2026), lililofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 27 Agosti 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC Jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo iliyopokelewa na Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Kaskazini Bi. Glory Kombe kwa niaba yake imelenga kutambua mchango alionao katika Sekta ya Mazingira hasa ikizingatiwa suala la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini ndio msingi wa Maendeleo endelevu kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.

Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hiyo, Naibu Waziri Mhe. Mboja Mshenga amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha juhudi za Uhifadhi na Usimamizi wa mazingira ya bahari, kwani ndio msingi wa maendeleo katika sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu huku akisistiza maendeleo ya kiuchumi ili kuhakikisha rasilimali za bahari zinalindwa na kutumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae

NEMC imeshiriki kongamano hilo kwa lengo la kuwasilisha na kujadili masuala ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira hususani Bahari kwa ustawi wa uvuvi na uchumi wa buluu endelevu.

Kongamano hilo lililowakutanisha wataalamu na wadau wa masuala ya bahari kutoka ndani na nje ya Tanzania, lililenga kujadili tafiti, ubunifu na teknolojia zinazoweza kuchangia maendeleo endelevu ya sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com