Na Mwandishi wetu, Dodoma
Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mhe, Alhaji Jabir Shekimweri amekipongeza chuo kikuu ardhi kwa kazi kubwa wanayoifanya ya ufundishaji vijana na kuandaa wataalamu wajao wataoleta tija kwa taifa.
Mhe. Shekimweri ameyasema hayo leo tarehe 6 Agosti 2026 alipotembelea banda la ARU katika maonyesho ya 33 ya kimataifa ya kilimo ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Mhe, Alhaji Shekimweri amesema kuwa uongozi wa chuo Pamoja na waalimu kwaujumla wanafanya kazi kubwa sana ya kufundisha vijana, na amejifunza kuwa kila mwaka una malengo yake katika ufundishaji, na ndipo wataalamu huanza kupikwa kuanzia mwaka wa kwanza na kuendelea ili kupata wataalamu waliobobea zaidi katika fani husika.
“Kama inavyotambulika kuwa kazi kuu za vyuo ni kufundisha, utafiti na ushauri wa kitaalamu, utafiti ni matokeo ya ufundishwaji kwa wanafunzi wa chuo husika, hivyo basi kutokana na tafiti na bunifu hizi za wanafunzi wa ARU nipongeze sana uongozi mzima wa chuo kikuu ardhi,Pamoja na timu nzima ya waalimu kwani wanafanya kazi kubwa sana ya kuwapika vijana hawa, na matokeo ndo haya tunayaona, nao wanafanya mambo makubwa kwenye tafiti na bunifu” alisema Mhe, Alhaji Shekimweri
Pia Mhe, Alhaji Shekimweri alisema kuwa yupo tayari kushirikiana na mwanafunzi wa chuo kikuu ardhi anaetengeneza mbolea kwa kutumia nywele za binaadamu kwa kununua bidhaa hiyo ila pia kumuunganisha na vinyozi wa Dodoma mjini ili kupata malighafi ya utengenezaji bidhaa hiyo.


Social Plugin