Na Ssgt Mawazo Mtondo - DODOMA.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, amesema kuwa Jeshi la Magereza linaendelea kutekeleza jukumu la kutoa hifadhi salama kwa wafungwa na mahabusu, sambamba na kuwasaidia kubadili mienendo na tabia kupitia elimu, mafunzo ya ufundi na stadi za maisha zitakazowawezesha kujitegemea pindi watakapomaliza vifungo vyao na kurejea katika jamii wakiwa raia wema.
Ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo, Agosti 3, 2026, Msalato Jijini Dodoma.
CGP. Katungu amesema, mchakato wa urekebishaji unalenga kuwajengea wafungwa maadili, ujuzi na uwezo wa kujitegemea, hatua inayochangia kupunguza uwezekano wa kurudia makosa na kuimarisha usalama wa jamii.
Amesisitiza kuwa Jeshi la Magereza linaendelea kutekeleza wajibu wake wa urekebishaji kwa kuzingatia misingi ya sheria, utu na haki za binadamu, huku likiwaandaa wafungwa kurejea katika jamii wakiwa na mchango chanya kwa maendeleo ya Taifa.



Social Plugin