Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limeelekeza kasi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, likisisitiza taasisi zinazotekeleza miradi kuhakikisha fedha zinapopatikana zinaelekezwa haraka kwenye utekelezaji ili wananchi wapate huduma kwa wakati.
Msisitizo huo umetolewa Agosti 4, 2026 katika kikao cha mkutano wa baraza la madiwani la kupokea na kujadili taarifa za Kata kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026, kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Enock Reuben, ambapo Baraza lilipongeza timu ya Mkurugenzi na menejimenti yake pamoja na taasisi za TARURA, RUWASA na TANESCO kwa hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto za wananchi.
Akijibu hoja za madiwani wa Kata za Bubiki, Bunambiyu, Talaga na Itilima, Mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi. Hussein Shaweji, amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027 serikali kupitia TARURA imeendelea kuhakikisha inaboresha miundombinu ya barabara kupitia fedha zinazopatikana kwenye vyanzo mbalimbali.
Akijibu hoja za madiwani wa Kata za Bubiki, Bunambiyu, Talaga na Itilima, Mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi. Hussein Shaweji, amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027 serikali kupitia TARURA imeendelea kuhakikisha inaboresha miundombinu ya barabara kupitia fedha zinazopatikana kwenye vyanzo mbalimbali.
Makamo Mwenyekti wa Halmasahuri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Enock Reuben ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za Kata kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika Agosti 4,2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
"TARURA imetenga Shiling bilioni 1.005 kutoka Mfuko wa Barabara kwa ajili ya ukarabati wa barabara katika Kata za Kishapu, Bunambiyu, Mwamashele, Mwaduhi-Lohunbo, Sekebugoro, Mwataga, Talaga, Uchunga, Igaga, Ngofila na Maganzo. Aidha, zimetengwa bilioni 1.425 kwenye fedha za tozo ya mafuta zitakazotumika katika Kata za Shagihilu, Itilima, Mwamalasa, Ukenyenge, Kishapu, Masanga, Mwasubi, Mwakipoya na Bunambiyu" amesema Shaweji
Mhandisi Shaweji ameongeza kuwa kupitia fedha za jimbo yaan Constutution Fund imetengwa kiasi cha Shilingi milioni 475 zikitumika kufanya marekebisho kwenye barabara za Ikonda–Mwaweja na Mwigumbi–Mpumbula.
Akijibu maswali kuhusu upanuzi wa miradi ya maji safi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA wilayani humo Mhandisi. Dickson Kamazima amesema mwaka huu wa fedha 2026/2027 taasisi hiyo imepanga kuendeleza na kukamilisha miradi mbalimbali.
Kamazima amesema miradi itakayotekelezwa ni ile ya zamani ambayo haikukamilika katika mwaka wa fedha uliopita na wameibua miradi mingine mitano (5) mipya ikiwa ni pamoja na Mradi wa maji Mpumbula -Mwigumbi (Milion 450), Mradi wa kuchimba kisima na kujenga kituo Mwagalankulu (Milioni 100), Mradi wa kuchimba kisima na kujenga kituo Mwalata (Milioni 100), Kuboresha chanzo cha maji Mwandoma (Milioni 50) pamoja na upanuzi wa mradi wa maji Kishapu- Mwanulu (Milioni 240)
"Miradi ya awali ambayo haikukamilika kutokana na sababu mbalimbali ni pamoja na Mradi wa Mwabusiga (Milion 208), Upanuzi wa mradi wa maji Nyenze (Milion 228), Ujenzi wa mradi wa maji Igaga (Milioni 506) na Ukamilishaji wa mradi wa maji Masanga-Ndoleleji (Milioni 891)." Ameongeza Kamazima
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapy mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za Kata kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika Agosti 4,2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Kamazima amekiri kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa maji katika maeneo ya Ikoma, Itilima na Ikonokelo akisema maeneo hayo yataendelea kutafutiwa fedha. Akieleza kuwa kwa Ngofila–Idushi, shirika la WorldVision ambae ndie mfadhili atasaidia upatikanaji wa maji katika eneo la Idushi na RUWASA kusaidia usambazaji wake.
Kwa upande wa Umeme, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Wilaya ya Kishapu Neema Robert ameeleza mikakati inayotekelezwa kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma hiyo baada ya Madiwani kuhoji hatua iliyofikiwa katika miradi ya REA iliyoongezwa katika baadhi ya vijiji na vitongoji, wakieleza kuwa wataalamu walishafika kufanya upimaji na kuweka alama kwenye baadhi ya maeneo, lakini utekelezaji haujaendelea huku baadhi ya wananchi tayari wameshafanya maandalizi ya kutumia nishati hiyo wakitarajia kuunganishwa. Baraza limemtaka mkandarasi wa REA kuhakikisha fedha zitakapotolewa aingie kwenye utekelezaji wa haraka ili wananchi wasiendelee kusubiri huduma.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed, amehimiza utekelezaji wa miradi kupewa kasi na kuhakikisha fedha zinazotengwa zinabadilika kuwa huduma halisi kwa wananchi. Amesema ushirikiano wa taasisi zote ni muhimu katika kuhakikisha changamoto zinazowasilishwa kupitia taarifa za Kata zinapatiwa majibu ya vitendo, huku Baraza likisisitiza kuwa mafanikio ya miradi hayapimwi kwa fedha kutengwa pekee, bali miradi kukamilika, huduma kuwafikia wananchi na changamoto kupungua ama kuondoka kabisa.
Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za Kata kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika Agosti 4,2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Kwa upande wa vyama vya siasa, Katibu wa ACT Wazalendo Wilaya ya Kishapu, Njile Nkuba, amewapongeza Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuwasemea wananchi na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata zao. Amesema mijadala inayofanyika katika Baraza la Madiwani ni muhimu kwa sababu inatoa fursa ya kuibua changamoto zinazowakabili wananchi, hususan katika huduma za afya, maji, barabara na umeme, huku akiwataka madiwani kuendelea kushirikiana na wananchi pamoja na taasisi za serikali ili kuhakikisha hoja zinazowasilishwa zinapata majibu na utekelezaji wa haraka.
Mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhandisi. Hussein Shaweji akijibu maswali ya Madiwani kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za Kata kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika Agosti 4,2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhandisi Dickson Kamazima akijibu maswali ya Madiwani kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za Kata kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika Agosti 4,2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Wilaya ya Kishapu Neema Robert wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akijibu maswali ya Madiwani kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za Kata kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika Agosti 4,2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Njile Nkuba akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za Kata kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika Agosti 4,2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Kaimu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Regina Athmani Ndulu akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama hicho wilaya kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili taarifa za Kata kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika Agosti 4,2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Social Plugin