Na Sheila Ahmadi, Dodoma
Kampuni ya Fair ago Enterprises imetoa pongezi Kwa Shoroba za ukuaji wa kilimo Tanzania (AGCOT) kwa kuweza kutoa mchango mkubwa kwenye kampuni hiyo ambayo imewezesha kufanya mkakati wa kuwafikia wakulima wadogo kwa karibu zaidi kupitia ushirikiano na vyama vya ushirika vya wakulima (AMCOS), kwa lengo la kuwawezesha kupata kwa urahisi pembejeo, teknolojia na huduma mbalimbali zinazohitajika katika uzalishaji wa kilimo.
Akizungumza na Wanahabari Kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji Wa Kampuni hiyo Suleiman Faraji amesema kuwa kupitia Shoroba za ukuaji wa kilimo Tanzania (AGCOT)Imewezesha kampuni hiyo kuchangia katika mabadiliko ya sekta ya kilimo kwa kuhakikisha wakulima wanapata huduma na bidhaa bora karibu na maeneo yao ya uzalishaji.
kupitia ubia na wadau mbalimbali, Fair ago inalenga kuanzisha maduka ya pembejeo katika maeneo ambayo yana mkusanyiko mkubwa wa wakulima, hususani maeneo yanayozungukwa na AMCOS.
Kupitia mchango huo uliofanywa na (AGCOT) maduka hayo yatamwezesha mkulima kupata mahitaji muhimu ya kilimo, ikiwemo dawa, mbegu na pembejeo nyingine, bila kulazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma hizo.
“Tunataka kufungua maduka yetu katika maeneo ambayo wakulima wanapatikana kwa wingi kupitia AMCOS, ili mkulima aweze kupata kila kitu anachohitaji, kuanzia dawa, mbegu na pembejeo nyingine,” amesema.
Aidha Mbali na huduma za pembejeo, Faraji ameongeza Fair Agro imejikita katika uzalishaji wa miche bora kwa lengo la kuwasaidia wakulima kuondokana na changamoto ya kuzalisha miche wenyewe na kupata hasara kutokana na makosa yanayoweza kujitokeza katika hatua za awali za uzalishaji.
Katika hatua nyingine kampuni hiyo inaendelea na mradi mkubwa wa uzalishaji wa miche ambao unalenga kuwa miongoni mwa vituo vikubwa vya uzalishaji wa miche nchini Tanzania.
Katika uzalishaji wa miche bora utasaidia kuongeza tija kwa wakulima wa mboga na mazao mbalimbali, huku ukiwawezesha kuanza uzalishaji kwa kutumia miche yenye ubora unaoweza kutoa matokeo mazuri shambani.
Vilevile wakulima wanaonunua miche kutoka kampuni hiyo pia watanufaika na mfumo wa punguzo la bei za pembejeo, ambapo wanaweza kupata punguzo la hadi asilimia tano kwa bidhaa zinazohusiana na uzalishaji wa mazao hayo.
“Tunataka kuhakikisha mkulima ananufaika zaidi. Anapochukua miche kwetu, anaweza pia kupata punguzo kwenye bidhaa tunazouza zinazohusiana na uzalishaji wa mazao hayo,” amesema.
Hata hivyo kampuni hiyo imeanza kuhamasisha matumizi ya kilimo cha ndani, ikiwemo greenhouse, akisema teknolojia hiyo inaweza kusaidia wakulima kukabiliana na changamoto za hali ya hewa na wadudu, pamoja na kuongeza ubora wa mazao.
uzoefu wa kampuni hiyo katika uzalishaji wa mazao kama nyanya umeonesha umuhimu wa kutumia teknolojia za kisasa katika kilimo, hasa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mahitaji ya soko.
Vilevile kilimo hapa Tanzania ni pamoja na kuangalia kilimo cha ndani, kama greenhouse, kwa sababu teknolojia hii inasaidia katika kudhibiti wadudu, hali ya hewa na kuhakikisha tunapata mazao yenye ubora unaohitajika sokoni,” amesema.
Nitoe Wito Kwa Serikali kuendelea kuandaa maonesho ya Nanenane, kwani yamekuwa jukwaa muhimu la kuwaunganisha wakulima na teknolojia, elimu pamoja na fursa mbalimbali katika sekta ya kilimo.
Sanjari na hayo maonesho hayo yanampa mkulima fursa ya kujifunza mbinu mpya za uzalishaji na kupata maarifa yanayoweza kumsaidia kuongeza tija katika shughuli zake.
wakulima Waendelee kutumia fursa zinazopatikana katika maonesho hayo na kuwa tayari kupokea teknolojia mpya ili kuongeza tija na kufanya kilimo kuwa shughuli yenye manufaa zaidi.
“Ujumbe wangu kwa wakulima ni kuhakikisha wanakuwa tayari kujifunza na kutumia teknolojia katika kilimo. Tukifanya hivyo, matokeo yataonekana na tutafikia transformation tunayohitaji katika sekta ya kilimo,” amesema Mkurugenzi Faraji".

Social Plugin