Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Jesca Simuchile, ameachia rasmi wimbo mpya unaoitwa "Ndoa Iheshimiwe", ukiwa ni kazi inayobeba mafundisho ya kibiblia yanayohimiza jamii kuilinda na kuiheshimu taasisi ya ndoa kama msingi wa familia na jamii.
Kupitia wimbo huo, Jesca anasisitiza umuhimu wa upendo, uaminifu, uvumilivu na heshima kati ya wanandoa, akiwakumbusha waumini kuishi kwa kufuata mafundisho ya Neno la Mungu kuhusu ndoa.
Mbali na ubora wa sauti, video rasmi ya "Ndoa Iheshimiwe" imeandaliwa kwa kiwango cha kimataifa cha 4K na imewekewa tafsiri za lugha ya Kiingereza (English Subtitles), hatua inayopanua wigo wa kufikisha ujumbe wa Injili kwa watazamaji wa mataifa mbalimbali wasioweza kuzungumza Kiswahili.
Kazi hiyo inaonyesha dhamira ya Jesca Simuchile ya kutumia muziki kama chombo cha kuhubiri Injili, kufundisha maadili ya Kikristo na kuimarisha taasisi ya familia kupitia ujumbe unaojenga na kuleta matumaini.
Baada ya mafanikio ya nyimbo zake zilizopita, zikiwemo "Tuimbe Tumepona" aliyomshirikisha Mwinjilisti Daniel Safari pamoja na "Neema Ingalipo," Jesca anaendelea kuthibitisha uwezo wake wa kuandika na kuwasilisha nyimbo zenye maudhui yanayogusa maisha ya kila siku ya Mkristo.
"Ndoa Iheshimiwe" sasa inapatikana kupitia YouTube, ambapo Jesca anawaalika waumini na wapenzi wa muziki wa Injili kuitazama, kushiriki ujumbe wake na kuendelea kumuunga mkono kwa kujisajili kwenye chaneli yake ili kupata kazi zake mpya.
Tazama video hapa chini


Social Plugin