Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC MBONI MHITA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM, 'RAIS SAMIA AMETOA TRILIONI 1.9 SHINYANGA'



Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa kipindi cha kuanzia Novemba, 2025 hadi Juni 2026.

TAZAMA VIDEO👇👇

Amewasilisha taarifa hiyo leo kwa Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mabala Mlolwa.

Mhita akisoma taarifa hiyo, amesema kwa kipindi cha uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wamepokea kiasi cha fedha sh. Trilioni 1.9 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.
Amesema, katika mapokezi ya fedha hizo wananchi wa Mkoa huo, wameshuhudia maendeleo ya haraka katika Nyanja za uzalishaji katika sekta ya kilimo, mifugo, madini, viwanda , biashara, pamoja na huduma za jamii, Afya, Elimu, Nishati na Maji.

UTEUZI WA VIONGOZI

Amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kumteuwa Mheshimiwa Patrobas Katambi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani na Mheshimiwa Salome Makamba kuwa Naibu Waziri wa Nishati.


WASIFU WA MKOA

Amesema mkoa huo wa Shinyanga una ukubwa wa kilomita za mraba elfu 18,557 na unajumla ya watu milioni 2,2 wanaume wakiwa milioni 1.102 na wanawake milioni 1.13 kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2022.
HALI YA UCHUMI YA MKOA

Amesema, mkoa huo umeendelee kuimarika ambapo pato halisi limeongezeka kutoka sh. bilioni 7.5 mwaka 2021 hadi sh.bilioni 9.2 mwaka 2026 sawa na ukuaji wa asilimia 22.

PATO LA MTU MMOJA

Amesema, pato la mtu mmoja mmoja limeongezeka kutoka sh. Milioni 1.8 mwaka 2021 hadi Sh.milioni 1.9 mwaka 2026 sawa na ongezeko la asilimia 7.

SEKTA YA AFYA

Amesema katika kuendelea kuimarisha sekta ya afya mkoa huo umepokea kiasi cha fedha sh. bilioni 99.0 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya.

Kukamilisha hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo iliyopo Mwawaza, kwa kujenga majengo ya EMD, OPD, Jengo la utawala, Jengo la Uraibu wa Madawa ya kulevya na kituo cha tiba jumuishi, kununua vifaa tiba, ujenzi wa nyumba za watumishi pamoja na kuongezeka kwa madawa na vitendanishi.

ELIMU

Amesema, katika kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote Mkoa huo umepokea sh. bilioni 205.2 kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu na kuongeza idadi ya walimu.

MAJI

Katika kuimarisha upatikanaji wa maji kwa wananchi wote kwamba mkoa huo umepokea sh. bilioni 163.3 ili kuhakikisha kaya nyingi zinaunganishwa na huduma ya maji, na kwamba upatikanaji wa maji kwa wananchi kwa sasa ni asilimia 79 kutoka 63 kwa maeneo ya mijini na vijijini asilimia 68 kutoka 51.

KILIMO

Kwamba wameendelea na ujenzi wa Skimu za bwawa la Nyida na Melenge, kuimarisha huduma za ugani kwa kununua vitendea kazi ikiwamo Pikipiki, vipima udongo na vishikwambi.

MIFUGO

Wameongeza usambazaji wa dawa za ruzuku za kuogeshea mifugo, kuimarisha huduma ugani kwa kugawa pikipiki 534 kwa ajili ya maafisa mifugo, pamoja na kuongeza minada ya mifugo kutoka 25 hadi 30.

MADINI

Kuongezeka kwa utoaji wa lessen kwa wachimbaji wadogo kutoka lesseni 332 hadi 1,766.

MIUNDOMBINU

Kuongezeka kwa mtandao wa barabara za lami kwa kilomita 57 ,barabara za changarawe kilomita 454, na kukamilika kwa ujenzi wa madaraja 18 ,makaravati 2,113, na pamoja na kuendelea kwa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kahama- Bulyanhulu kilomita 73 kwa gharama ya sh.bilioni 100.6 na ujenzi umefikia asilimia 78.21.

NISHATI

Amesema Rais Dk Samia ametoa bilioni 426 kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini, pamoja kuendelea kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme jua katika kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu kwa kuzalisha Megawati 100 kwa awamu ya pili.

UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

Kuongezeka kwa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo kiasi cha sh. bilioni 11.3 zimetolewa kwa vikundi 941 vya wanawake, Vijana 599 na watu wenye ulemavu vikundi 110.

TASAF

Zimetolewa fedha sh. bilioni 59.5 kwa walengwa elfu 35,055 kutekeleza miradi 77 ya miundombinu ya elimu, afya, barabara, pamoja na kuwezesha walengwa elfu 15,103 kujiongezea kipato kupitia ufugaji na kilimo.

UTAWALA BORA

Mkoa umepokea bilioni 22,2 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala na nyumba za watumishi, katika Hamashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga DC, Ushetu na ujenzi wa Jengo la Ofisi ya mwendesha Mashtaka.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesema wamempongeza Mkuu huyo wa mkoa kwa usimamizi mzuri wa fedha za serikali na kuitendelea haki ilani ya uchaguzi ya Chama hicho.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kipindi cha kuanzia Novemba 2025 hadi Juni 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kipindi cha kuanzia Novemba 2025 hadi Juni 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kipindi cha kuanzia Novemba 2025 hadi Juni 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kipindi cha kuanzia Novemba 2025 hadi Juni 2026.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza,

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com