Mtendaji Mkuu wa Geita Gold FC, Gilbert John, na Mkuu wa Ubunifu, Mikakati na Chapa wa Jambo Group ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Jambo Media Group, Nickson George, wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Geita Gold FC na Jambo Group kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027. Picha na Elizabeth Cosmas
Mtendaji Mkuu wa Geita Gold FC, Gilbert John, na Mkuu wa Ubunifu, Mikakati na Chapa wa Jambo Group ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Jambo Media Group, Nickson George (kulia), wakitia saini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Geita Gold FC na Jambo Group kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027.
Mtendaji Mkuu wa Geita Gold FC, Gilbert John, na Mkuu wa Ubunifu, Mikakati na Chapa wa Jambo Group ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Jambo Media Group, Nickson George, wakionesha mikataba ya ushirikiano wa kimkakati baada ya kusaini makubaliano kati ya Geita Gold FC na Jambo Group kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027.
Na Elizabeth Cosmas, Malunde 1 Blog – Shinyanga
Kampuni ya Jambo Group imeingia makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati na klabu ya Geita Gold FC kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027, hatua inayolenga kukuza sekta ya michezo, kuimarisha biashara na kuongeza utangazaji wa bidhaa za Jambo katika Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza leo Julai 28,2026 wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ushirikiano huo, Mkuu wa Ubunifu, Mikakati na Chapa wa Jambo Group ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Jambo Media Group, Nickson George, amesema makubaliano hayo ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo wa kusogeza bidhaa zake karibu zaidi na wananchi kupitia nguvu ya michezo.
Amesema ushirikiano huo umebebwa na kaulimbiu ya "Kocha wa Dhahabu", ambayo inaashiria mwanzo wa safari mpya kati ya Jambo Group na Geita Gold FC.
"Leo tunakuja na kaulimbiu ya 'Kocha wa Dhahabu', ambayo inabeba maana kubwa ya kuanzisha ushirikiano rasmi na Geita Gold FC. Lengo letu ni kuendelea kutangaza bidhaa zetu katika maeneo yote ya Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla," amesema George.
Naye Mtendaji Mkuu wa Geita Gold FC, Gilbert John, ameishukuru Jambo Group kwa kuiongeza klabu hiyo katika familia ya washirika wake, akisema ushirikiano huo utaendelea kujenga mahusiano mazuri kati ya pande hizo mbili katika sekta ya michezo na biashara.
Amesema uwepo wa Jambo Group ndani ya Geita Gold FC utasaidia pia kuongeza nguvu ya utangazaji wa bidhaa za kampuni hiyo katika Kanda ya Ziwa na maeneo mengine ya jirani.
"Tunamshukuru Jambo Group kwa kutuongeza kwenye familia yake. Tunaamini ushirikiano huu utakuwa na manufaa makubwa kwetu, hasa katika kukuza michezo lakini pia kusaidia bidhaa za Jambo kuendelea kufanya vizuri zaidi katika maeneo mbalimbali," amesema Gilbert.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Geita Gold FC, Zengo Pole, amesema ushirikiano huo unaonyesha namna sekta ya michezo inavyoendelea kuwaunganisha wadau mbalimbali na kujenga familia kubwa ya maendeleo.
Amesema kuongezeka kwa wadhamini na washirika katika klabu hiyo kutasaidia kukuza mchezo wa soka na kuleta manufaa kwa pande zote zinazohusika.
"Ushirikiano huu ni hatua muhimu kwetu kwa sababu unaonyesha namna michezo inavyoweza kuunganisha wadau mbalimbali kwa ajili ya maendeleo," amesema Pole.
Hatua hii inakuja ikiwa ni mwendelezo wa uwekezaji wa Jambo Group katika michezo nchini, ambapo kampuni hiyo pia imeongeza mwaka mwingine wa udhamini kwa klabu ya Dodoma Jiji FC baada ya kusaini mkataba mpya wa ushirikiano kwa msimu wa 2026/2027 ikiwa ni dhamira kubwa ya Jambo Group kuendelea kuunga mkono ukuaji wa soka nchini na kujenga mahusiano ya kimkakati na klabu mbalimbali kwa manufaa ya michezo, biashara na jamii kwa ujumla.
Mtendaji Mkuu wa Geita Gold FC, Gilbert John, na Mkuu wa Ubunifu, Mikakati na Chapa wa Jambo Group ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Jambo Media Group, Nickson George, wakionesha mikataba ya ushirikiano wa kimkakati baada ya kusaini makubaliano kati ya Geita Gold FC na Jambo Group kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027.
Mtendaji Mkuu wa Geita Gold FC, Gilbert John, na Mkuu wa Ubunifu, Mikakati na Chapa wa Jambo Group ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Jambo Media Group, Nickson George, wakitambulisha jezi mpya ya Geita Gold FC yenye nembo ya Jambo Group baada ya kuingia makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027.






















Social Plugin