Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VISIMA 362 VIMECHIMBWA KWA AJILI YA UMWAGILIAJI NCHINI - NIRC



Na Sheila Ahmadi, Dodoma

Tume ya umwagiliaji (NIRC) Imeendelea kutekeleza miradi ya uchimbaji wa visima nchini ambapo kwa sasa visima 362 vimechimbwa kwenye mikoa ya Manyara, Geita,Singida na tabora lengo la uchimbaji wa visima hivyo ni kuhakikisha wakulima wanazalisha mazao kwa wakati.

Hayo yamesemwa Mkoani dodoma Na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji (NIRC)Bi Maria itembe kwenye Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma ambapo amesema Tunaendelea kusimamia ujenzi wa Miundombinu na uchimbaji wa visima kwenye maeneo yenye ukame ili kwenda kuongeza upatikanaji wa maji kwa ajili ya kilimo cha Umwagiliaji.

Aidha Bi Maria ameongeza kuwa Kupitia Maadhimisho hayo tunatoa elimu mbalimbali kwa wananchi wanaotembelea kwenye banda letu ili waendelee kufahamu tume hiyo inavyofanya kazi.

"Tume yetu ina programu ya uchimbaji wa visima ambavyo vinatumia Mitambo ya kisasa hivyo inawawezesha wakulima kuzalisha mazao mengi kwa wakati Muafaka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa tafiti na msimamizi wa uchimbaji visima kutoka kwenye tume hiyo Bi Naomi Mcharo ameongeza kuwa serikali imeanzisha huduma ya uchimbaji wa visima vya umwagiliaji katika kuendeleza uchumi na maendeleo ya nchi na kuwafikia wakulima wengi nchini.

Tume ya Umwagiliaji inashirikiana na Halmashauri zote za wilaya nchini katika kutambua na kuhakiki vikundi vya wakulima ambavyo vinanufaika na programu hiyo huku kila wilaya ikianza na visima vitano katika hatua ya kwanza.

Hata hivyo Wakulima binafsi wenye mashamba kuanzia hekari 20 hadi 40 wanaweza kuwasilisha maombi kwa tume ili kuchimbiwa visima kwa utaratibu maalumu unaojumuisha ruzuku ya asilimia 20 ya garama za uchimbaji.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com