Na mwandishi wetu
Vijana mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya Mkoa wa Dar Es Salaam, wanaofanya shughuli za kuokota makopo, kuosha magari pamoja na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu, wameeleza kuhusu athari za maandamano kiusalama na kijamii, wakitahadharisha kwamba ni muhimu kukataa vishawishi mbalimbali vinavyoelekezwa kwa Vijana ili kuweza kushiriki katika matukio ya uvunjifu wa amani pamoja na maandamano yanayohamasishwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa yatafanyika Julai 07, 2027.
Bw. Mohamed Salehe, Kijana anayeokota makopo eneo la Kijitonyama, Jijini hapa amebainisha kuwa licha ya yeye kufanya kazi asiyoipenda ila bado kupitia amani iliyopo Nchini ameweza kuendelea kujipatia kipato kupitia shughuli hiyo, akisema wakati wa ghasia za Oktoba 2025, alishindwa kumudu mahitaji muhimu kutokana na kushindwa kutoka kwenda kuokota makopo mitaani.
"Wanasiasa wanaokuja kwetu na kusema tuandamane tuwaambie hapana. Kama vijana tusiwakubali hawa wanasiasa wanaotujaza sumu ili kututaka tuandamane, hizo sio siasa, siasa zinapaswa kufanyika kwa amani na utulivu.' Amesema Bw. Salehe.
Kwa upande wake Bw. Kevin Shinyaka, anayeosha magari kwenye eneo la Sinza, ameeleza kuwa kando ya kupoteza ndugu zake wakati wa ghasia za Mwezi Oktoba, kingine alichojifunza ni kuwa maandamano yamekuwa na tija kwa watu wachache na wasioshiriki maandamano husika, akibainisha uwepo wa serikali na kutaka kila mwenye changamoto kubisha hodi kwenye Ofisi za Serikali kutafuta muafaka wa kero walizonazo.
Wakihitimisha mazungumzo yao, Bw. Sadati Mzala, Kijana anayeishi Ubungo Dar Es Salaam, ameungana na Vijana wengine kote Nchini kusisitiza kuhusu umuhimu wa amani Nchini, akihimiza Vijana kutoshawishika na mitandao ya kijamii na badala yake wajifunze kutoka kwenye Mataifa yasiyokuwa na amani ili kuona namna watu wanavyotaabika.



Social Plugin