Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANIA YASHIRIKI JUKWAA LA UTALII, BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MISRI


Cairo, Misri,

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi leo Juni 8, 2026 ameshiriki Ufunguzi wa Jukwaa la Utalii, Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri linalofanyika jijini Cairo, likiwakutanisha viongozi wa Serikali, taasisi za utalii, wafanyabiashara, wawekezaji na wadau mbalimbali kutoka nchi hizo mbili kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kukuza fursa za biashara, uwekezaji na utalii.

Jukwaa hilo limeandaliwa chini ya kaulimbiu inayohamasisha uhusiano kati ya Bahari ya Mediterania na Bahari ya Hindi kupitia masoko, utalii, biashara na uwekezaji, likitoa fursa kwa wadau kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano yenye manufaa kwa pande zote mbili.

Katika jukwaa hilo, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki mjadala ambapo washiriki walijadili fursa za ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Misri.

Aidha, washiriki walipata fursa ya kushuhudia video mbalimbali za kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na kufanya mikutano ya kibiashara (B2B) na majadiliano yaliyolenga kuanzisha na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau wa sekta binafsi kutoka Tanzania na Misri.

Jukwaa hilo limehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dennis Londo, Naibu Waziri wa Utalii na Mambo Kale Misri, Mhe. Yomna El Bahar, Balozi wa Tanzania nchini Misri Meja Jenerali Richard Makanzo na viongozi wengine mbalimbali wa Serikali kutoka nchi zote mbili.

Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Sofitel jijini Cairo, Misri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com