Na Sumai Salum- Kishapu
Shirika la Tanzania Christian Refugee Service (TCRS) limetambulisha Mradi wa Ustahimilivu Jumuishi wa Jamii katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi utakaotekelezwa katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kwa ufadhili wa Shirika la Finnish Evangelical Lutheran Mission (FELM) kwa fedha kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland.
Akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi huo Juni 24, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mratibu wa Miradi wa TCRS Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Oscar Rutenge, amesema mradi huo unalenga kuimarisha ustahimilivu wa jamii dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kuongeza usalama wa chakula, kuinua kipato cha wananchi na kuimarisha uhifadhi wa mazingira.
Amesema mradi huo utatekelezwa katika vijiji 10 vya Kata za Talaga na Itilima kwa kipindi cha miaka minne, huku ukilenga kujenga uwezo wa wananchi kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi kupitia mbinu mbalimbali za maendeleo endelevu.
“Mradi huu utalenga kuongeza usalama wa chakula, kuboresha kipato cha wananchi, kuimarisha uhifadhi wa mazingira na kuwezesha jamii kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,” ameongeza Dkt. Rutenge.
Aidha, Dkt. Rutenge amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Emmanuel Johnson, kwa ushirikiano unaotolewa na Halmashauri katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Josephat Limbe Akizungumza wakati akifungua kikao cha kutambulisha Mradi wa Ustahimilivu Jumuishi wa Jamii katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wenye Thamani ya Tsh. Bilioni 1.064 unaotekelezwa na shirika la TCRS kwa Kata ta Talaga na Itilima Juni 24, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Josephat Limbe, amesema TCRS ni mdau muhimu wa maendeleo ambaye amekuwa akishirikiana na Halmashauri kwa muda mrefu katika kupeleka huduma kwa wananchi wa kata mbalimbali za wilaya hiyo.
Amesema pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri na fedha zinazotolewa na Serikali Kuu, mchango wa wadau wa maendeleo una nafasi kubwa katika kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuharakisha maendeleo ya jamii.
“Ushirikiano wa wadau wa maendeleo kama TCRS unaisaidia Serikali kufikisha huduma kwa wananchi kwa haraka zaidi na kupunguza changamoto zinazowakabili katika maeneo mbalimbali,” ameongeza Limbe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Johnson, akizungumza kwenye kikao cha kutambulisha Mradi wa Ustahimilivu Jumuishi wa Jamii katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wenye Thamani ya Tsh. Bilioni 1.064 unaotekelezwa na shirika la TCRS kwa Kata ta Talaga na Itilima Juni 24, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Josephat Limbe, amesema TCRS ni mdau muhimu wa maendeleo ambaye amekuwa akishirikiana na Halmashauri kwa muda mrefu katika kupeleka huduma kwa wananchi wa kata mbalimbali za wilaya hiyo.
Amesema pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri na fedha zinazotolewa na Serikali Kuu, mchango wa wadau wa maendeleo una nafasi kubwa katika kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuharakisha maendeleo ya jamii.
“Ushirikiano wa wadau wa maendeleo kama TCRS unaisaidia Serikali kufikisha huduma kwa wananchi kwa haraka zaidi na kupunguza changamoto zinazowakabili katika maeneo mbalimbali,” ameongeza Limbe.
Mradi huo unaotekelezwa kwa fedha zenye thamani ya Tshilingi bilioni 1.064 unatarajiwa kunufaisha maelfu ya wananchi wa vijiji kumi vilivyoko Kata ya Talaga na Itilima kupitia shughuli zitakazochochea maendeleo ya kiuchumi, uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.
Social Plugin