
Bariadi, Simiyu.
Mwanamke maarufu katika sekta ya madini, Salma Mipawa, ametunukiwa Tuzo ya Mwanamke Shupavu wa Sekta ya Madini na Uchimbaji katika hafla ya Mwanamke Shupavu Lake Zone 2026 iliyofanyika mjini Bariadi, Mkoa wa Simiyu.
Tuzo hiyo imetolewa na HOLYSMILE kwa lengo la kutambua mchango wake mkubwa katika maendeleo ya sekta ya madini, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na jitihada zake za kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika shughuli za uzalishaji na maendeleo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa HOLYSMILE, Arnold Bweichum (HolySmile), alisema kuwa Salma Mipawa ameendelea kuwa mfano wa mwanamke jasiri, mchapakazi na mwenye maono ambaye ameonyesha uwezo mkubwa wa kuleta matokeo chanya katika sekta ya madini.
“Tunatambua mchango wake mkubwa katika kukuza sekta ya madini na kuhamasisha wanawake wengi kuona kuwa wanaweza kushiriki kikamilifu katika sekta hii muhimu ya uchumi wa taifa. Tuzo hii ni ishara ya kuthamini kazi kubwa anayoifanya,” alisema HolySmile.
Kupitia tuzo hiyo, HOLYSMILE imeeleza kuwa inalenga kuhamasisha wanawake wengine kuendelea kutumia vipaji, maarifa na nafasi walizonazo kuleta maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.
Hafla ya Mwanamke Shupavu Lake Zone 2026 imewakutanisha wanawake kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kutambua mafanikio yao, kujenga mtandao wa ushirikiano na kuhamasisha maendeleo ya wanawake katika sekta tofauti.
Kutunukiwa kwa Salma Mipawa kumepokelewa kwa furaha na washiriki wa hafla hiyo, huku wengi wakieleza kuwa ni miongoni mwa wanawake walioonyesha uongozi, uthubutu na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya madini nchini.
Imetolewa na:
HOLYSMILE
Tunatambua na Kuthamini.














Social Plugin