Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KILOGRAMU 109,206 ZAUZWA MNADA WA TANO WA TAMCU LTD.

Mwenyekiti wa Mruji AMCOS kutoka katika kijiji cha Mchesi Omari Mohamed Ally akizungumza kuhusu kuridhishwa na bei ya ufuta iliyofanyika leo tarehe 16 juni 2026 katika kijiji hicho cha Mchesi kata ya Mchesi Tarafa ya Lukumbule Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma

Kaimu Mwenyekiti wa TAMCU LTD Kaisi Rashid Makolela alieshika maiki akitaja bei ya zao la ufuta katika mnada uliofanyika leo tarehe 16 juni 2026 katika kijiji cha Mchesi Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma huku bei ya juu ya ufuta huo ikiwa shilingi 2260 na bei ya chini ikiwa ni shilingi 2250.






























Na Regina Ndumbaro Tunduru-Ruvuma 


Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU) LTD kimeendelea na mnada wake wa tano wa zao la ufuta, uliofanyika leo Juni 16, 2026 katika kijiji cha Mchesi, kata ya Mchesi, Tarafa ya Lukumbule, Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. 


Katika mnada huo, jumla ya kilogramu 109,206 za ufuta kutoka Kikundi cha Ushirika cha Mruji AMCOS ziliuzwa, huku bei ya juu ikiwa Sh 2,260 kwa kilo, bei ya chini Sh 2,250 na bei ya wastani ikiwa Sh 2,255 kwa kilo.

Mwenyekiti wa Mruji AMCOS, Omari Mohamed Ally, amesema wakulima wamekubali kuuza mazao yao kwa bei hiyo kutokana na hali halisi ya soko pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoshuhudiwa kwa sasa. 


Amesema upepo wa soko si mzuri kama ilivyokuwa katika minada iliyopita, hivyo hawajashangazwa na kiwango hicho cha bei.


Ameongeza kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika masoko, matarajio ya wakulima ni kuona bei za zao la ufuta zikiendelea kuongezeka ili kuongeza kipato na kuimarisha ustawi wa kaya zinazotegemea kilimo hicho.


Kwa upande wao, wakulima wa kijiji cha Mchesi wameeleza kuridhishwa na bei ya wastani ya Sh 2,255 kwa kilo. 


Mkulima Juma Hassan Juma amesema wakulima wamekubaliana na bei hiyo, huku akiitaka Serikali kuangalia uwezekano wa kuongeza asilimia ya motisha kwa wakulima ili kuhamasisha zaidi uzalishaji na uuzaji wa zao la ufuta.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com