Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC GLORIANA KIMATH AKAGUA MIRADI ITAKAYOTEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU JULAI 8, 2026 MONDULI

Na Mwandishi wetu, Monduli.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Gloriana Kimath, akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT), ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopendekezwa kutembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 8 Julai 2026.

Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Mradi wa Vijana wa Umoja Group uliopo Mto wa Mbu, Kijiji cha Barabarani; Mradi wa Foot on Africa Safari Lodge uliopo Kijiji cha Majengo, Kata ya Majengo; Mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na madawati katika Shule ya Sekondari Migungani One, Kata ya Migungani; Mradi wa Maji wa Laiboni uliopo Kata ya Esilalei; Mradi wa matumizi ya Nishati Mbadala katika Shule ya Sekondari Alfa na Omega, Kijiji cha Sinoni Ngarash, Kata ya Engutoto; pamoja na Mradi wa Jengo la Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli, Kata ya Monduli Mjini.

Mhe. Kimath amesisitiza marekebisho madogo yaliyobainika katika miradi hiyo kufanyiwa kazi kwa wakati ili kuhakikisha ipo tayari kabla ya ujio wa Mwenge wa Uhuru.

Aidha, Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 zinatarajiwa kuingia Mkoa wa Arusha tarehe 5 Julai 2026 na kukimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli tarehe 8 Julai 2026.

Mwenge wa Uhuru 2026 umebeba kaulimbiu isemayo: "Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com