Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kupata kichwa cha aliyekuwa mwanafunzi wa IFM, James Temba, ambaye hivi karibuni mwili wake ulikutwa ukielea kwenye maji ya Mto Msimbazi nakuzikwa Mkoani Kilimanjaro.
Akizunguma Mei 13, 2026 jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Aidha, amesema kuwa baada ya upelelezi wa kina kufanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya uchunguzi wa kisayansi, sehemu ya kichwa hicho imepatikana eneo la Kitunda Kibeberu, Wilaya ya Ilala, kikiwa kimefukiwa ardhini.
“Hadi sasa watu watano wamekamatwa, akiwemo mganga wa kienyeji anayejulikana kwa jina la Saidi Ally (Side) Mzigua (31),” amesema SACP Muliro.
Na kuongeza kuwa, “Taratibu za kisheria zinakamilishwa ili watuhumiwa wafikishwe kwenye mamlaka za kisheria.”
Aidha, amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwashukuru wananchi na mamlaka nyingine za uchunguzi wa kisayansi katika kufanikisha zoezi la upatikanaji wa kichwa hicho.
“Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuacha kutoa taarifa za upotoshaji wakati uchunguzi wa matukio ya kihalifu, ikiwemo mauaji, unaendelea.”
Hata hivyo, Jeshi hilo linaendelea kulaani watuhumiwa waliotekeleza mauaji hayo na kwamba litaendelea kufuatilia jalada la kesi hiyo ili watuhumiwa wapate adhabu wanayostahili

Social Plugin