Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DED MBEYA DC AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA AJIRA 259.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Bi. Erica E. Yegella amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fursa ya ajira mpya takriabani 259 katika kipindi cha mwezi Januari na Mei 2026.

Katika kipindi cha mwezi Januari, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ilifanikiwa kupangiwa ajira mpya takribani 111 kwenye kada tofauti tofauti ikiwemo elimu msingi na sekondari, afya, ujenzi, maendeleo ya jamii, utawala, na mawasiliano.

Mnamo mwezi Aprili 2026, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ilipangiwa ajira mpya 118 kwenye kada tofauti tofauti ikiwemo elimu msingi na sekondari, afya, ujenzi, na uhasibu.

Mwezi Mei, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ilipangiwa ajira mpya 30 mahususi kwa ajili ya watu wa kada ya afya pekee, wakataosaidia jitihada za utoaji huduma muhimu za afya katika zahanati na vituo vya afya vilijengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Bi. Yegella amesema ajira mpya zilizotolewa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, ni jambo ambalo anapaswa kupongezwa sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukubali ombi la kuongeza watumishi katika Halmashauri.

"Katika kipindi cha miezi mitano pekee, Rais ameruhusu Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kupangiwa ajira mpya zaidi ya 250. Tunamshukuru sana kwa hili. Hii ni fursa kwa vijana wa kitanzania pamoja Halmashauri kwani itasaidia kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma muhimu za kijamii," ameeleza Bi. Yegella.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com