Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ukenyenge iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameeleza mafanikio yaliyopatikana baada ya kuanzishwa kwa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto ndani na nje ya Shule.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mei 29,2026 wakati wa kikao maalumu cha kufuatilia mwenendo wa Dawati hilo, kilichoratibiwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali Nchini Rafiki-SDO lenye makao yake makuu Mjini Shinyanga, Mwanafunzi wa kidato Cha pili shuleni hapo Constantine Peter na Eveline Samweli wa Kidato cha tatu wamesema uwepo wa Dawati la watoto umepelekea uhai wa sanduku la maoni na kufanya wanafunzi kueleza changamoto zao bila hofu.
Wamesema hatua hiyo imechangia kupungua kwa baadhi ya vitendo vya ukatili na matumizi ya adhabu kali za viboko, huku wanafunzi wakipewa nafasi ya kusikilizwa na kushirikishwa katika masuala yanayowahusu.
Aidha wameeleza kuwa dawati hilo limekuwa msaada mkubwa katika kujenga mahusiano mazuri kati ya wanafunzi, walimu na jamii kwa ujumla, jambo ambalo limeongeza hali ya amani na utulivu shuleni.
Akizungumza katika kikao hicho, Meneja na Mratibu wa Mradi kutoka Shirika la Rafiki-SDO mkoani Shinyanga, George Nyamboto amesema ikiwa ni miezi mitatu sasa takribani tangia kuanzishwa kwa Dawati hilo katika Wilaya ya Kishapu wameanza kuona mafanikio chanya katika ulinzi na usalama wa watoto.
Amesema lengo la kikao hicho ni kutathmini maendeleo ya Dawati hilo, kujadili changamoto zilizopo pamoja na kuweka mpango kazi wa namna ya kuzitatua kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wa elimu.
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Ukenyenge wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Eveline Samweli akizungumza wakati wa kikao maalumu cha kufuatilia mwenendo wa Dawati hilo, kilichoratibiwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali Rafiki-SDO mkoani humo Mei 29,2026 walipokuwa Shule ya Sekondari Ukenyenge
George ameongeza kuwa uwepo wa dawati hilo umeongeza ushirikishwaji wa wanafunzi katika mambo yanayowagusa moja kwa moja, hali ambayo ni chachu ya kuleta mabadiliko chanya na kusaidia kuondoa migomo, migogoro pamoja na vitendo vinavyoweza kusababisha madhara au uharibifu wa mali za umma shuleni.
"Pamoja na mambo mengine muongozo wa serikali unataka masanduku haya ya maoni yawekwe mahali panapofikika, penye usalama na lifunguliwe mara tatu kwa juma ikiwa ni siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa na tunaimani shule itatekeleza hivyo ili kuendelea kubaini changamoto bado Iko wapi na jinsi gani tunashirikiana na serikali yetu sikivu kuitatua kupitia vyombo vyake vilivyopewa Mamlaka" ameongeza Nyamboto
Pia amesema, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya shule kwa kuhakikisha watoto wanakuwa salama wawapo mashuleni kupitia uanzishwaji wa jukwaa hilo muhimu, huku akiwataka wanafunzi kuwa mawakala wa mabadiliko kwa wenzao kwa kuzingatia nidhamu na kuongeza bidii katika masomo.
Mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Ukenyenge wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Constantine Peter akizungumza wakati wa kikao maalumu cha kufuatilia mwenendo wa Dawati hilo, kilichoratibiwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali Rafiki-SDO mkoani humo Mei 29,2026 walipokuwa Shule ya Sekondari Ukenyenge.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mei 29,2026 wakati wa kikao maalumu cha kufuatilia mwenendo wa Dawati hilo, kilichoratibiwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali Nchini Rafiki-SDO lenye makao yake makuu Mjini Shinyanga, Mwanafunzi wa kidato Cha pili shuleni hapo Constantine Peter na Eveline Samweli wa Kidato cha tatu wamesema uwepo wa Dawati la watoto umepelekea uhai wa sanduku la maoni na kufanya wanafunzi kueleza changamoto zao bila hofu.
Wamesema hatua hiyo imechangia kupungua kwa baadhi ya vitendo vya ukatili na matumizi ya adhabu kali za viboko, huku wanafunzi wakipewa nafasi ya kusikilizwa na kushirikishwa katika masuala yanayowahusu.
Aidha wameeleza kuwa dawati hilo limekuwa msaada mkubwa katika kujenga mahusiano mazuri kati ya wanafunzi, walimu na jamii kwa ujumla, jambo ambalo limeongeza hali ya amani na utulivu shuleni.
Akizungumza katika kikao hicho, Meneja na Mratibu wa Mradi kutoka Shirika la Rafiki-SDO mkoani Shinyanga, George Nyamboto amesema ikiwa ni miezi mitatu sasa takribani tangia kuanzishwa kwa Dawati hilo katika Wilaya ya Kishapu wameanza kuona mafanikio chanya katika ulinzi na usalama wa watoto.
Amesema lengo la kikao hicho ni kutathmini maendeleo ya Dawati hilo, kujadili changamoto zilizopo pamoja na kuweka mpango kazi wa namna ya kuzitatua kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wa elimu.
George ameongeza kuwa uwepo wa dawati hilo umeongeza ushirikishwaji wa wanafunzi katika mambo yanayowagusa moja kwa moja, hali ambayo ni chachu ya kuleta mabadiliko chanya na kusaidia kuondoa migomo, migogoro pamoja na vitendo vinavyoweza kusababisha madhara au uharibifu wa mali za umma shuleni.
"Pamoja na mambo mengine muongozo wa serikali unataka masanduku haya ya maoni yawekwe mahali panapofikika, penye usalama na lifunguliwe mara tatu kwa juma ikiwa ni siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa na tunaimani shule itatekeleza hivyo ili kuendelea kubaini changamoto bado Iko wapi na jinsi gani tunashirikiana na serikali yetu sikivu kuitatua kupitia vyombo vyake vilivyopewa Mamlaka" ameongeza Nyamboto
Pia amesema, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya shule kwa kuhakikisha watoto wanakuwa salama wawapo mashuleni kupitia uanzishwaji wa jukwaa hilo muhimu, huku akiwataka wanafunzi kuwa mawakala wa mabadiliko kwa wenzao kwa kuzingatia nidhamu na kuongeza bidii katika masomo.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ukenyenge Mwl. Majige Magembe mbali na kuipongeza jitihada za serikali na Shirika la Rafiki-SDO, amewasisitiza wanafunzi kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya ukatili mbalimbali wanavyoviona au kuvipitia katika jamii zao ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa mapema.
"Jukwaa hili tunaona limesaidia kuleta mabadiliko kwa wanafunzi wetu kwanza kuwa wazi katika yote wanayoona wanafanyiwa ukatili, limewapa kujitambua na hivyo tunaamini ufaulu utaongezeka zaidi" ameongeza Majige.
Aidha amewatahadharisha wanafunzi dhidi ya utovu wa nidhamu na kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi wakiwa shuleni, akiwataka kuzingatia masomo na kufuata malengo yao ya badae.
Mratibu wa dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto wilayani humo, Viridiana Bruno ameeleza changamoto ya baadhi ya watoto kuzuiwa kuhudhuria shule kwa ajili ya kazi za nyumbani au kuchunga mifugo, hali inayowakosesha muda wa kujisomea na kuathiri maendeleo yao ya kitaaluma, akisema kuwa hiyo ni miongoni mwa ukatili waopitia baadhi yao hivyo wanapaswa kupaza sauti endapo wakiona matukio hayo.
"Kuna ukatili mwingi huko kwenye jamii ambao watoto baadhi yao wamekuwa wakikutana nao na nyie tunatamani zaidi mjikite sio tu kusema ukatili mnaofanyiwa muwapo mashuleni Bali zaidi nje ya shule ili serikali iweze kuutokomeza na mbakie kuwa salama" ameongeza
Kutoka Shirika la Rafiki-SDO Queen Gerald amewasisitiza wanafunzi kuepuka vitendo vinavyoweza kuwa vikwazo kwa maendeleo yao ya elimu ikiwa ni pamoja na utoro, kutohudhuria vipindi na vitendo vingine kama hivyo.
Social Plugin