Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia : MAMA MZAZI WA HAYATI MAGUFULI AFARIKI DUNIA

Mama Mzazi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, ambaye ni Suzana Magufuli, amefariki dunia mjini Chato mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli, aliyesema kuwa Bibi Suzana amefariki nyumbani kwake Chato na kwamba familia itaendelea kutoa taarifa kuhusu taratibu za msiba huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com