Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHADEMA KESHO WANANCHI WANATARAJIA MAREJEO YA HEKIMA NA UWAJIBIKAJI

Kwa mara ya kwanza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitakutana na waandishi wa habari katika mkutano ambao unasubiriwa kwa hamu kutokana na maendeleo ya siasa za Tanzania katika siku za karibuni.

Kwa wale wanaoipenda mama Tanzania Mkutano huu unaotarajiwa kufanyika kesho,unatarajiwa kuwa  wa weledi mkubwa na hakuna anayetarajia kuwepo na lugha za hamasa zinazoelekeza kwenye vurugu nyingine. 

Taifa limeshaona na kuonja hasara kubwa ya vurugu kama zile za Oktoba 29, ambazo zilisababisha upotezaji wa maisha ya Watanzania, majeraha, na uharibifu wa mali. 

Tayari maneno yapo mtaani lakini ni matumaini ya wengi kwamba badala ya kukataa Ripoti ya Tume ya Jaji Chande, tunatarajia kuona mkikubali matokeo ya uchunguzi huo wa kisayansi na kuchukua hatua za kujiimarisha ndani kwa kukemea udhalilishaji wa viongozi wa kitaifa na taifa lenyewe huko mtandaoni.

Ni imani yetu na matumaini ya Watanzania kuwa mkutano huu utakuwa ni fursa ya kutoa mwelekeo chanya wa mambo mliyoyajadili katika vikao vyenu, mkijikita zaidi katika ujenzi wa amani, umoja, na mustakabali wa Taifa letu.

Ni jambo jema kuwasikia tena mkirejea katika shughuli zenu za kisiasa baada ya kipindi ambacho shughuli za chama zilionekana kusuasua kutokana na changamoto za kisheria mlizokuwa nazo ndani ya chama. 

Tutafurahi kama wananchi walioonja  shubiri kuwa kesho maelezo yatakayotolewa  yatakuwa yenye tija na yenye kulinda amani ya nchi.

Kwa kuwa Watanzania hawataki kuishi kwa wasiwasi, kesho tunatarajia kusikia maamuzi ya kikao chenu yanayojenga amani badala ya mbinu za kutupa lawama kwa wengine wakati ukweli wa mchango wenu katika hali ya sasa unajulikana. Taifa letu linahitaji hekima, si jazba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com