Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAMIA WAJITOKEZA MAZISHI YA MZEE MAARUFU 'BUTTA ISACK TUNGU GIMU' KIJIJINI ZOBOGO

Mamia ya waombolezaji wamejitokeza katika kijiji cha Zobogo, Kata ya Itwangi wilayani Shinyanga kushiriki mazishi ya Mzee Maarufu Butta Isack Tungu Gimu aliyefariki dunia Mei 26, 2026 akiwa na umri wa miaka 92.

Mazishi hayo yamefanyika Mei 28,2026 katika makaburi ya familia yaliyopo katika kijiji cha Zobogo kata ya Itwangi.
Butta alikuwa kiongozi maarufu katika jamii ambapo amewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Tawi la Zobogo, Mjumbe wa Baraza la Mahakama ya Mwanzo Itwangi, Balozi wa Nyumba Kumi lakini pia amekuwa Mzee wa Kanisa la Anglikana Parish ya Zobogo hadi alipofariki dunia.

Waombolezaji waliomzungumzia marehemu wamesema alikuwa mtu mwenye hekima, upendo na mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii.

Butta aliyezaliwa mwaka 1934 na kufariki dunia Mei 26,2026 akiwa Mjini Kahama wakati akipelekwa Hospitali ya Manispaa ya Kahama akisumbuliwa na changamoto ya kifua na presha ameacha mjane, watoto 9, wajukuu 52, vitukuu 103 pamoja na vilembwe 7.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com