Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UTENDAJI KAZI WA TADB WAMFURAHISHA WAZIRI MKUU


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa mchango wake katika kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi kupitia utoaji na usimamizi wa mikopo, hatua aliyoeleza kuwa inaendelea kuchochea maendeleo ya sekta za uzalishaji na ukuaji endelevu wa uchumi wa Taifa.

Pongezi hizo amezitoa leo Mei 28, 2026 jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambapo taasisi mbalimbali zimekutana kuonesha mchango wao katika maendeleo na uhifadhi wa mazingira.

TADB ni miongoni mwa taasisi zilizoshiriki katika maadhimisho hayo.

Maadhimisho hayo yameambatana na maonyesho pamoja na Kongamano la wadau wa mazingira ili kuimarisha usimamizi wa mazingira kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni Tunza Mazingira, Linda Taifa hayo yote yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com