Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VIJANA SIMAMENI KIDETE KULINDA UMOJA NA AMANI YA TANZANIA- DKT. NCHIMBI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa Vijana na Taifa kwa ujumla kusimama kidete katika kulinda umoja, kujenga uadilifu kwa mtu mmoja mmoja, Taasisi na Taifa kwa ujumla pamoja na kuimarisha misingi ya kujitegemea kiuchumi, kiakili na kimaamuzi ili kuijenga Tanzania.

Makamu wa Rais ametoa rai hiyo wakati wa kongamano la Vijana katika kumbukizi ya Miaka 104 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Chimwaga Mkoani Dodoma, akibainisha umuhimu wa Kila kijana kutambua wajibu wa msingi wa kizazi chao kwa kuhakikisha wanashiriki katika ujenzi wa Tanzania yenye amani, uadilifu na yenye kujitegemea.

"Ni wito wangu kwamba tusimame na tuseme kwamba tutaulinda umoja wetu kwa nguvu zetu zote, tusimame tuseme tutajenga uadilifu kwa mtu mmoja mmoja na kwa Taasisi zetu, tusimame na tuseme tutatumia elimu na ubunifu wetu katika kukuza maendeleo ya nchi yetu. Tusimame na tuseme tutafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuimarisha misingi ya kujitegemea kiuchumi, kiakili na kimaamuzi ili kuijenga nchi yetu." Amekaririwa Dkt. Nchimbi.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais pia amemshukuru Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere pamoja na wote aliofanya nao kazi katika kipindi chake cha uongozi, akisema Viongozi hao walifanya kazi nzuri ya kujenga misingi imara ya Tanzania, akihimiza utayari wa Viongozi wa sasa katika kuendeleza mazuri yenye mchango wa maendeleo kwa Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com