Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SAIDI ANAPIGANIA MAISHA YAKE – ANAHITAJI UPASUAJI WA HARAKA, MSAADA WAKO NI TUMAINI LAKE




Ndugu zetu wa Malunde Blog,

Hali ya ndugu yetu Saidi Mikidadi Abdallah bado ni mbaya, na kwa sasa amelazwa hospitalini akipatiwa matibabu. Madaktari wameeleza kuwa anahitaji kufanyiwa upasuaji wa haraka (surgery) siku ya Jumatatu ili kuokoa maisha yake.

Kwa masikitiko makubwa, hadi sasa gharama za matibabu bado hazijakamilika . 

Hii ina maana kuwa muda unaendelea kuyoyoma huku uhai wake ukiwa hatarini zaidi.

Familia inaendelea kupambana kwa kila hali, lakini ukweli ni kwamba hawawezi kumudu gharama peke yao. 

Ndiyo maana tunakuomba wewe, ndugu, rafiki na mtu mwenye moyo wa huruma  usimame nasi katika wakati huu mgumu.

Kila mchango wako, hata uwe mdogo kiasi gani, unaweza kuwa sababu ya kuokoa maisha ya Saidi.

Pamoja na msaada wa kifedha, tunaomba pia muendelee kumuombea kwa Mungu ampiganie katika kipindi hiki kigumu.

 Jinsi ya Kuchangia:

 Namba: 0757551443 (Vodacom)

 Jina: Radhia Rajabu

Mchango wako utasaidia kuleta tumaini jipya, faraja kwa familia, na zaidi ya yote  nafasi ya uhai kwa Saidi.

Tafadhali shiriki ujumbe huu uwafikie watu wengi zaidi. Leo unaweza kuwa sababu ya kesho ya mtu mwingine.

Tunawashukuru sana kwa upendo, dua na msaada wenu mnaoendelea kutupatia. Mungu awabariki sana.

Kila dakika ni muhimu,kila msaada una maana. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com