Na mwandishi wetu,Singida
Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), imeendesha mafunzo maalum kwa wachimbaji wadogo wa madini yenye lengo la kuongeza uelewa kuhusu uchimbaji salama, wenye tija na unaozingatia utunzaji wa mazingira.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea wachimbaji uwezo katika matumizi ya teknolojia bora za uchimbaji, usimamizi wa afya na usalama migodini, uongezaji thamani wa madini pamoja na kuimarisha biashara ya madini kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za sekta ya madini.
Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo, Mhandisi Sabai Nyansiri, amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wachimbaji wadogo ili kuhakikisha sekta ya madini inachangia kikamilifu maendeleo ya wananchi na uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kuongeza tija, kipato na kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia misingi ya usalama, uhifadhi wa mazingira na uendelevu wa rasilimali madini.



Social Plugin