Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA FUM KISHAPU YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA TSH. BILIONI 1.2

Na Sumai Salum- Kishapu

Katika jitihada za kuhakikisha fedha za umma zinaleta matokeo chanya kwa wananchi, Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imefanya ziara maalum ya kukagua miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 1, 278,000,000.


Ziara hiyo imefanyika Aprili 15 hadi 16, 2026, ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Enock Reuben, ambapo wajumbe wa kamati walitembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.


Miradi iliyokaguliwa inagusa moja kwa moja maisha ya wananchi, ikiwemo miradi ya afya, umeme wa jua, ujenzi wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo kwenye baadhi ya zahanati na maegesho ya magari mnada wa Mhunze, ujenzi wa nyumba mpya ya Mkurugenzi Mtendaji, ujenzi wa vichomea taka katika zahanati, pamoja na maendeleo ya kikundi cha Vijana na Wanawake waliopewa mikopo ya asilimia 10 wa Halmashauri hiyo.


Kwa mujibu wa kamati hiyo, lengo kuu la ziara lilikuwa ni kufuatilia kwa karibu matumizi ya fedha za miradi, kutathmini hatua za utekelezaji, pamoja na kubaini changamoto zinazoweza kukwamisha ukamilishaji wa miradi hiyo.


Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mhe. Reuben amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kila shilingi ya umma inaleta thamani halisi kwa wananchi (value for money), huku akiwataka watendaji kusimamia miradi kwa weledi na uwajibikaji mkubwa.


Kamati haikuishia kukagua tu, bali pia ilitoa maelekezo na ushauri muhimu kwa watendaji. Miongoni mwa mambo yaliyosisitizwa ni, usimamizi makini wa fedha za miradi, uzingatiaji wa viwango vya ubora wa ujenzi, kukamilika kwa miradi ndani ya muda uliopangwa pamoja na utatuzi wa changamoto kwa wakati.


Hatua hizi zinalenga kuhakikisha miradi hiyo inaleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi bila kuchelewa wala kupoteza rasilimali.


Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ina nafasi muhimu katika kusukuma maendeleo ya wilaya. Kupitia ziara kama hizi, kamati inaendelea kuhakikisha uwajibikaji unaimarika, fedha zinatumika ipasavyo, na miradi inatekelezwa kwa ufanisi.


Kwa ujumla, ziara hii ni ishara ya dhamira ya dhati ya viongozi wa Kishapu katika kusimamia maendeleo na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazotokana na miradi hiyo.Makamo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na Diwani wa Kata ya Masanga Mhe. Enock Reuben akisikiliza maelezo kwenye ziara ya kamati ya Fedha Utawala na Mipango iliyofanyika Aprili 14-15, 2026 ya ukaguzi wa miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya Tsh. bilioni 1.2Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akiielezea jambo kamati ya Fedha Utawala na Mipango wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi 8 ya maendeleo yenye thamani ya Tsh. bilioni 1.2 Aprili 14-15, 2026 Diwani wa Kata ya Mwamalasa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Bushi Mpina ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wa Halmashauri ya wilaya hiyoDiwani wa viti maalumu Kata ya Ukenyenge Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Sophia Masele ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wa Halmashauri ya wilaya hiyoDiwani wa Kata ya Songwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Abdul Ngoromole ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wa Halmashauri ya wilaya hiyoDiwani wa Kata ya Kishapu Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wa Halmashauri ya wilaya hiyoPicha za Miradi






Tazama picha za matukio mbalimbali




































































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com