Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAKAMPUNI 100 KUSHIRIKI MAONESHO YA OSHA

Meneja wa OSHA Nyanda za juu Kusini Wilbert Ngowi

 Mtendaji Mkuu  Mkuu OSHA ,Khadija Mwenda

***

Na Mwandishi Wetu, Njombe

MAKAMPUNI zaidi ya 100 yakiwepo ya uchimbaji wa madini, yanatarajiwa kushiriki maonesho yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) yatakayofanyika uwanja wa sabasaba mjini Njombe.

Maonesho hayo, yanatarajiwa kufunguliwa rasmi April 24  viwanja vya Sabasaba na kilele chake kinatarajiwa kuwa April 29, ikiwa pia ni sehemu ya maadhimisho ya Usalama na afya sehemu za kazi Duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari kutoka chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) ambao wanashiriki maadhimisho ya kitaifa ya sherehe ya Mei mosi, Meneja wa OSHA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Wilbert  Ngowi amesema, maandalizi yote yamekamilika.

Ngowi amesema  licha ya uwepo wa maonesho hayo, ambayo pia yatapamba maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa, kuwa kuwa na utoaji wa tuzo  kwa makampuni na taasisi ambazo zinazingatia  Usalama na afya  kazini.

"Tunatarajia tuzo hizi zitatolewa April 29 katika ukumbi wa Agriment mjini Njombe na  mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu",amesema.

Ngowi amesema sambamba na Maonesho, OSHA imeandaa semina kwa wafanyakazi mkoani Njombe  kuhusiana na masuala ya kazi, afya na Saikolojia April 27 lakini pia kutakuwa na michezo mbalimbali .

"Tumejipanga vizuri katika maadhimisho haya ya Mei Mosi mwaka huu na tunaimani yatafana sana na tunatoa wito makampuni ambayo bado hayajakamilisha taratibu za ushiriki yajitokeze kujisajili kupitia mfumo wa OSHA", amesema.

Chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) kwa mara ya kwanza mwaka huu kinashiriki pia maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa mkoani Njombe na katika baadhi ya mikoa nchini.

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com