Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ASKOFU DKT. MNDOLWA APONGEZA KUUNDWA KWA TUME YA OKTOBA 29 "NI UKOMAVU WA NCHI



Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dkt. Mahimbo Mndolwa amesema kuundwa kwa Tume huru ya kuchunguza matukio ya Uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 ni tendo la ukomavu na busara na maamuzi sahihi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuipeleka Tanzania sehemu sahihi.

Askofu Mndolwa amebainisha hayo mapema leo Jumatatu Aprili 13, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam kuelekea kukabidhiwa kwa ripoti ya Tume hiyo kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza pia kufurahishwa na namna ambavyo Tanzania ilichukua hatua ya kushughulikia changamoto zake wenyewe badala ya kuchukua Vyombo na watu kutoka nje ya nchi kama ilivyokuwa ikishurutishwa na baadhi ya watu na Taasisi mbalimbali.

"Kiukweli kwa aina ya watu tulionao katika Tume ile ya Oktoba 29 tutaelekea sehemu sahihi kama Taifa na kwakweli tusiseme tu kwa Taifa, hata katika familia mgogoro ukizuka anzeni kwanza ninyi wenyewe kama maandiko yanavyotutaka kusemezana na ndugu zako pale mnapokosana kwahiyo kwa kuanza na sisi ndio ukomavu wenyewe kwamba hatushindwani, tunaonekana Taifa huru na kweli ni kuwa tumeshaweza." Amesema Askofu Mndolwa.

Kiongozi huyo wa kiroho amemshukuru Mungu kwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali na Watanzania katika utatuzi wa kero na changamoto zilizopo nchini, akisema kwa uzoefu wa vikao mbalimbali ambavyo wamekuwa wakishiriki kimataifa, wamesisitiza kwamba Tanzania haijashindwa katika utatuzi wa kero na changamoto zilizopo za kijamii na kiuchumi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com