Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAGANGA WA TIBA ASILI WAJIWEKA SAWA KUNOLEWA NA MKEMIA MKUU


Katibu Mkuu wa TAMESOT, Lukas Mlipu, (wa tatu kutoka kushoto, mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na waganga wa tiba asili na tiba mbadala mkoani Geita.
Na Theophilida Felician – Geita

Waganga wa tiba asili na tiba mbadala wanatarajia kukutana na Mkemia Mkuu wa Serikali ili kupatiwa elimu thabiti itakayowawezesha kuendelea kutoa huduma sahihi kwa jamii.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini (TAMESOT), Bw. Lukas Joseph Mlipu, alipokuwa katika Kata ya Butengorumasa mkoani Geita akiwahamasisha waganga kuhusu umuhimu wa kushiriki mafunzo yatakayotolewa na Mkemia Mkuu wa Serikali.

Amesema mafunzo hayo yanayowalenga waganga wote yana umuhimu mkubwa kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili taaluma ya tiba asili. Ameeleza kuwa juhudi za serikali, ikiwemo utoaji wa elimu kwa wataalamu hao, zitasaidia kuboresha huduma za tiba asili na kuhakikisha zinaendeshwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu.

Aidha, Bw. Mlipu amefafanua kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali atatoa mafunzo hayo tarehe 23 Machi, 2026, mkoani Geita. Hivyo, ametoa wito kwa waganga wote kuhakikisha hawakosi fursa hiyo muhimu kwa mustakabali wa taaluma yao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com